Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe,Abdalla
Mwinyi Khamis,(katikati) akitoa nasaha zake kwa wanafamilia wa
Marehemu Koplo Said Abdulrahman Juma Hassan wa Jeshi la POLISI
,alipofika kukabidhi fedha kwa ajili ya Ubani kwa Niaba ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,nyumbani kwa wafiwa Nyerere Mjini Zanzibar leo ,wengine
kushoto Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Ali Mwema,
(kushoto) na kutoka kulia Kamishna wa Polisi Zanzibar MUssa Ali Mussa
na Afisa Tawala Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahamoud,),hafla
hiyo ilifanyika leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe,Abdalla
Mwinyi Khamis,(kulia) akikabidhi fedha kwa ajili ya Ubani kwa Niaba ya
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,nyumbani kwa wafiwa wa Marehemu Koplo Said Abdulrahman Juma
Hassan wa Jeshi la Polisi, Nyerere Mjini Zanzibar leo ,kwa niaba ya
wanafamilia wa marehemu Baba Mdogo Juma Omar Salum,(wa pili
kushoto),akipokea ubani, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said
Ali Mwema,(wa pili kulia) na Baba Mzani wa Marehemu,Abdulrahman Juma
Hassan,(kushoto).
Kumkalisha jamvini kamanda wa Polisi akiwa amevaa gwanda kabisa kweli hii inakubalika?
ReplyDeleteFedha hazito ziba pengo lililowachwa na marehemu. cha msingi ni kufuata sheria na katiba ktk kutimiza wajibu wenu jeshi la polisi kwa kufanya hivyo mengi yanaweza epukika ikiwamo vifo vya namna hii, manung uniko na hali ya kutoridhika inayoonyshwa na wananchi juu yenu. Umekuwa utaratibu wa kawaida sasa kutoa fedha au kutembelewa wafiwa na wakubwa kwa lengo la kufunika mambo flani flani hali ya kua ukweli utabaki ukweli milele.
ReplyDeleteJamani muwe mnatufahamisha kuhusu huyu marehemu Koplo Said amefanya nini mpaka umauti umfikie.Yaani tunaomba info zake maana mnaandika mazishi yake lakini hakuna habari zozote.
ReplyDeleteheee basi wewe Anony saidi, sii mfatilia habari naona leo ndo kwanza kwako kumekucha kama wewe ni mtanzania inabidi ubadilike kwani siku nyingine utambiwa Tanzania imeuzwa na sii tanzania tena utabaki unashangaaa hamka please???
ReplyDeleteMdau wa tatu hapo juu Mon Oct 29, 10:53:00 PM 2012
ReplyDelete...Jamani muwe mnatufahamisha kuhus huyu marehemu Koplo Said amefanya nini mpaka umauti umfike...
JIBU NI HILI:
KOPLO SAID ABDULRAHMAN AMEJITOA MAISHA YAKE KIUTETEA NCHI AMEKWENDA MBELE ZA HAKI SASA BADO ZAMU YAKO WEWE MDAU UNAETAKA KUJUA TAARIFA ANGALIA NA WEWE UFANYE KITU GANI KUIPIGANIA NCHI ?
wewe anon wa kwanza, kwa ni nani alomlazimisha huyo kamanda kwenda mazikoni na magwanda yake? waislamu tukifiwa tunakaa jamvini, tabia zilizoanzishwa na baadhi ya watu katika miaka ya hivi karibuni ya kukaa vitini sio yetu na sio kila mmoja anaekubaliana nayo. Nimefurahishwa sana na familia ya marehemu ya kudumisha desturi za kukaa jamvini wakati wa msiba.
ReplyDelete