Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe,Abdalla Mwinyi Khamis,(katikati) akitoa nasaha zake kwa wanafamilia wa Marehemu Koplo Said Abdulrahman Juma Hassan wa Jeshi la POLISI ,alipofika kukabidhi fedha kwa ajili ya Ubani kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,nyumbani kwa wafiwa Nyerere Mjini Zanzibar leo ,wengine kushoto Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Ali Mwema, (kushoto) na kutoka kulia Kamishna wa Polisi Zanzibar MUssa Ali Mussa na Afisa Tawala Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahamoud,),hafla hiyo ilifanyika leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe,Abdalla Mwinyi Khamis,(kulia) akikabidhi fedha kwa ajili ya Ubani kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,nyumbani kwa wafiwa wa Marehemu Koplo Said Abdulrahman Juma Hassan wa Jeshi la Polisi, Nyerere Mjini Zanzibar leo ,kwa niaba ya wanafamilia wa marehemu Baba Mdogo Juma Omar Salum,(wa pili kushoto),akipokea ubani, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Ali Mwema,(wa pili kulia) na Baba Mzani wa Marehemu,Abdulrahman Juma Hassan,(kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kumkalisha jamvini kamanda wa Polisi akiwa amevaa gwanda kabisa kweli hii inakubalika?

    ReplyDelete
  2. Fedha hazito ziba pengo lililowachwa na marehemu. cha msingi ni kufuata sheria na katiba ktk kutimiza wajibu wenu jeshi la polisi kwa kufanya hivyo mengi yanaweza epukika ikiwamo vifo vya namna hii, manung uniko na hali ya kutoridhika inayoonyshwa na wananchi juu yenu. Umekuwa utaratibu wa kawaida sasa kutoa fedha au kutembelewa wafiwa na wakubwa kwa lengo la kufunika mambo flani flani hali ya kua ukweli utabaki ukweli milele.

    ReplyDelete
  3. Jamani muwe mnatufahamisha kuhusu huyu marehemu Koplo Said amefanya nini mpaka umauti umfikie.Yaani tunaomba info zake maana mnaandika mazishi yake lakini hakuna habari zozote.

    ReplyDelete
  4. heee basi wewe Anony saidi, sii mfatilia habari naona leo ndo kwanza kwako kumekucha kama wewe ni mtanzania inabidi ubadilike kwani siku nyingine utambiwa Tanzania imeuzwa na sii tanzania tena utabaki unashangaaa hamka please???

    ReplyDelete
  5. Mdau wa tatu hapo juu Mon Oct 29, 10:53:00 PM 2012

    ...Jamani muwe mnatufahamisha kuhus huyu marehemu Koplo Said amefanya nini mpaka umauti umfike...

    JIBU NI HILI:

    KOPLO SAID ABDULRAHMAN AMEJITOA MAISHA YAKE KIUTETEA NCHI AMEKWENDA MBELE ZA HAKI SASA BADO ZAMU YAKO WEWE MDAU UNAETAKA KUJUA TAARIFA ANGALIA NA WEWE UFANYE KITU GANI KUIPIGANIA NCHI ?

    ReplyDelete
  6. wewe anon wa kwanza, kwa ni nani alomlazimisha huyo kamanda kwenda mazikoni na magwanda yake? waislamu tukifiwa tunakaa jamvini, tabia zilizoanzishwa na baadhi ya watu katika miaka ya hivi karibuni ya kukaa vitini sio yetu na sio kila mmoja anaekubaliana nayo. Nimefurahishwa sana na familia ya marehemu ya kudumisha desturi za kukaa jamvini wakati wa msiba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...