Mhe. Waziri Membe akifafanua kuhusu mgogoro wa Mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Uenyekiti wa Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mbeya wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani).
Wilayani Kyela, Mbeya
Mhe. Waziri Membe akiongea na Wajumbe wa msafara wake akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro (mwenye shati jeupe mbele ya Waziri), Balozi Irene Kasyanju (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Dkt. Mohamed Maundi (kushoto), Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia - Kurasini. (Picha hii na Mbaraka Islam)
Makazi ya wananchi wa Malawi kando ya Mto Songwe ambapo mmoja wa wananchi anaonekana akifua nguo (pichani - upande wa kushoto; ng'ando ya mpaka kwa upande wa Malawi) wakati wengine (kulia) wanaonekana wakiendelea na shughuli zao za kawaida huku wakiwa tayari wamevuka ng'ando ya mpaka kwa upande wa Tanzania. Picha, maelezo na Tagie Daisy Mwakawago
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Sio ng'ando..... Ni ng'aMbo.
ReplyDeleteNimeweka capital M kwa uwelewesho!
Kiswahili jamani kina wapiga chenga wengi mno na hasa wale ambao taaluma zao ni za uandishi.
Kiingereza cha tabu.... Sasa Watanzania kweli tumejitayarisha vya kutosha kwa soko hutia na makazi huria katika jumuia ya Afrika Mashariki.
Labda tutoe Wamachinga tu!
Mdau msahihishaji hapo juu sio hutia ni huRia! nimeweka herufi kubwa pia kwa makzo zaidi!
ReplyDeletetofautisha taipo na leksimu!
Mdau hapo juu nawe sio maKzo zaidi bali ni mKazo zaidi. Nafunga mjadala...hahahaa.
ReplyDelete