Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na ujumbe wake katika mazungumzo na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Ndugu Suleiman Saleh (wa pili kulia) yaliyolenga namna ya kuongeza idadi ya wageni kutoka Marekani kuja Tanzania. Wengine katika picha kutoka kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Paul Sarakikya, Katibu wa Waziri Egidius Mweyunge na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Dk. Simon Mduma.
 1.      Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (wa pili kushoto) na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ambapo wamefika kwa ajili ya mwaliko wa serikali ya Marekani kwa ajili ya kuangalia maeneo ya kushirikiana kiuhifadhi na uongezaji wa watalii kutoka Marekani. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Afisa wa Ubalozi Suleiman Saleh, Mhe. James Lembeli ambaye ni Mwenyekti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira, Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori Paul Sarakikya, Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dk. Simon Mduma na Katibu wa Waziri Egidius Mweyunge. 

1.      Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli wakiangalia vipeperushi mbalimbali vilivyopo katika ubalozi wetu nchini Marekani vinavyotumika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii nchini kwa wageni wanaofika ubalozini hapo.Habari Picha na Pascal Shelutete 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hiyo picha ya mh.kikwete na obama imegeuzwa ndio kama tishio hahahaha wa uswazi ni uswazi tu

    ReplyDelete
  2. Kagasheki umeona nchi inayofaa kutangaziwa utalii ni Marekani tu,hii si mara yako ya kwanza kuwa huko katika kipindi cha miezi sita,kwani hakuna nchi nyingine za ulaya na Amerika ambazo zinaweza kutangaziwa utalii,lakini pili nashindwa kuelewa kazi za balozi zetu huko nje ikiwa Waziri ndo amekuwa na dhamana hiyo ya kwenda kutangaza utalii wetu.

    ReplyDelete
  3. Kama mnashindwa kutupa hata DVD watanzania za kuonyesha vivutio watanzania tulioko nje tuwaonyeshe wenyeji wetu, kweli mnaweza tangaza kwa njia nyingine?

    ReplyDelete
  4. Sasa wanatangaza utalii au wanatangaza Obama na Kikwete. kwani hiyo picha inahusikaje na utalii? Nafikiri watu wanaofanya hizi shughuli upeo ni mdogo sana...!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...