1.
Waziri wa Maliasili na
Utalii Balozi Khamis Kagasheki (wa pili kushoto) na ujumbe wake wakiwa katika
picha ya pamoja katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ambapo wamefika kwa
ajili ya mwaliko wa serikali ya Marekani kwa ajili ya kuangalia maeneo ya
kushirikiana kiuhifadhi na uongezaji wa watalii kutoka Marekani. Wengine katika
picha kutoka kushoto ni Afisa wa Ubalozi Suleiman Saleh, Mhe. James Lembeli
ambaye ni Mwenyekti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira, Kaimu
Mkurugenzi wa Wanyamapori Paul Sarakikya, Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dk. Simon
Mduma na Katibu wa Waziri Egidius Mweyunge.
1. Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli wakiangalia
vipeperushi mbalimbali vilivyopo katika ubalozi wetu nchini Marekani
vinavyotumika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii nchini kwa wageni
wanaofika ubalozini hapo.Habari Picha na Pascal Shelutete



hiyo picha ya mh.kikwete na obama imegeuzwa ndio kama tishio hahahaha wa uswazi ni uswazi tu
ReplyDeleteKagasheki umeona nchi inayofaa kutangaziwa utalii ni Marekani tu,hii si mara yako ya kwanza kuwa huko katika kipindi cha miezi sita,kwani hakuna nchi nyingine za ulaya na Amerika ambazo zinaweza kutangaziwa utalii,lakini pili nashindwa kuelewa kazi za balozi zetu huko nje ikiwa Waziri ndo amekuwa na dhamana hiyo ya kwenda kutangaza utalii wetu.
ReplyDeleteKama mnashindwa kutupa hata DVD watanzania za kuonyesha vivutio watanzania tulioko nje tuwaonyeshe wenyeji wetu, kweli mnaweza tangaza kwa njia nyingine?
ReplyDeleteSasa wanatangaza utalii au wanatangaza Obama na Kikwete. kwani hiyo picha inahusikaje na utalii? Nafikiri watu wanaofanya hizi shughuli upeo ni mdogo sana...!!
ReplyDelete