Kijana ambaye jina lake halikufakamika mara moja akiwa amebeba lumbesa ya Makopo ya Maji ya Plastiki  yaliyokwisha tumika,tayari kwa kwenda kuyapima na kuyauza kwa wahusika.Biashara hii ya Makopo ya Maji yaliyotumika imekuwwa ikipunguza kwa kiasi kikubwa sana hali ya Uchafuzi wa Mazingira katika maeneo mbali mbali ya Jiji letu,kwani hata ukitupa hovyo,basi jua kuna mtu atapita kuchukua muda mchache tu ujao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hapo zamani nakumbuka kuwa watu waliokuwa wanaokota makopo tuliwaita machizi, wamerukwa na akili, vichaa, n.k!

    Miaka ya leo kazi hiyo hiyo ni bonge la ajira!!

    Ama kweli dunai inabadirika!

    ReplyDelete
  2. Hii biashara ni ktk moja ya sekta muhimu za ajira na uwekezaji nchini Tanzania!

    ReplyDelete
  3. Ankali tulikwisha elewana kwa picha kama hizi:

    1.Yule jamaa aliyekuwa anakokota baiskeli akiwa miguu peku peku kwenye mlima akiwa na gunia 2 za mkaa tulipatana uandike ya kuwa yupo mbali na mji huko Kijijini ingawa inaonekana barabara ya Lami ni kuwa maendeleo sasa Bongo yamefikia lami hadi Vijijini!.

    2.Hii hapa jamaa akiokota chupa za maji tuseme yeye yupo Mjini na kuwa (hafanyi Kazi Ajira) au (Bishara ya Kuuza chupa tupu) ila yeye ni Wananchi wa kawaida ameamua kujitolea kusafisha mazingira!.

    Hii ni kujenga ili wandugu zetu Majuu wasije wakapata hofu ya kuwa labda Bongo sio Tambarale kuna shida hivyo wasije wakakataa kurudi!!!

    ReplyDelete
  4. Ahhh wapi!

    Huyo ni Pusha Alwatani sana maeneo ya Jangwani Mabondeni kule chini Klabu ya Yanga anaitwa 'Kijiti cha Mboka' Msela wa Tabora.

    Jamaa anazuga tu kujifanya anafaynya kazi ya kuokota chupa tupu huku akiwa Pusha, ili kuwakwepa Ulinzi Shirikishi na Maafisa wa Serikali ya Mtaa.

    Kwao ni Tabora na 'mizigo' anatumiwa na Babu yake kutoka huko (Mboka) yaani mkoani Isevya-Tabora!!!

    ReplyDelete
  5. Ahhh wapi!

    Huyo ni Pusha Alwatani sana maeneo ya Jangwani Mabondeni kule chini Klabu ya Yanga anaitwa 'Kijiti cha Mboka' Msela wa Tabora.

    Jamaa anazuga tu kujifnya anafaynya kazi ya kuokota chupa tupu huku akiwa Pusha, ili kuwakwepa Ulinzi Shirikishi na Maafisa wa Serikali ya Mtaa.

    Kwao ni Isevya-Tabora na 'mizigo' anatumiwa na Babu yake kutoka huko (Mboka) yaani Tabora!!!

    ReplyDelete
  6. Ohooo maisha ama kweli changamoto Mjini ndio kama hivi kula kwa tindo, Vijijini ndio hivyo tena mara kiangazi mara njaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...