Kaka naomba uitundike hii kuonyesha wazi kuwa huyu Cristiano Ronaldo si Muislam na ni Mkatoliki tena anavaa rozari ameweza kuondoa udini wake na kuweka mbele ubinadamu wake na kutoa pesa zake Euro milioni 1.5 kujenga shule zilizopo ukanda wa Gaza zilizopigwa mabomu na jeshi la Israel.

Hili ni fundisho toka kuwa sisi sote ni binadamu na ni changamoto kwa wanamichezo na wenye uwezo Tanzania kufuata nyayo za mchezaji kama Ronaldo. Kwa kiasi amenikumbusha George Weah wa Liberia kwa moyo mzuri alio nao.

Katika lindi la habari mbaya wiki nzima habari hii kwa kweli inatia sana moyo jinsi tulivyo wamoja kama binadamu.

Cristiano Ronaldo donates €1.5mn to children in Gaza


https://rt.com/sport/football/ronaldo-gaza-real-madrid-237/

http://www.koonis.com/wp-content/uploads/2011/11/falastiin.jpg


-Mdau, Wimbi la Mbele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Si ubinadamu tu bali ni kumcha mungu kweli. Maana Mungu hana dini wala dhehebu- si mwislamu wla mkristo wala Mluteri wala Moraviani wala Mkatoloki. Tukibagua kwa misingi hii hakika tumepotea maana tunaambiwa tumeumbwa kwa mfano wake.

    ReplyDelete
  2. Asante kwa taarifa nzuri. ILA naomba ufahamu kuwa Palestine siyo wote ni Waislam pale kuna Waislam na Wakristo. Palestine ni Mchanganyiko wa hizo dini mbili kubwa (Christians & Muslims). Vile vile napenda kukufahamisha kuwa Wayahudi siyo Wakristo ndiyo maana walikuwa wanampinga Yesu ambaye alikuwa Mkristo na hadi kesho hawaamini U-kristo. Kwahiyo usiuweke kabisa Uyahudi na Ukiristo katika kundi moja. Wale ni Wayahudi na kuna Wakrito na Waislam.

    ReplyDelete
  3. Bwana Asifiwe sana Kwa kitendo hiki cha Ronaldo.

    Nampongeza sana Ronaldo kwa Msaada huu muhimu sana kwa Wapalestina.

    ReplyDelete
  4. MUNGU WAEPUSHE WAPALESTINA (WAKRISTO, WAISLAMU, WASIO DINI N.K.) NA MATESO WANAYOYAPATA KUTOKA KWA WAYAHUDI

    MUNGU BWANA WA VIUMBE WA DUNIA HII, WAKUMBUSHE WAYAHUDI MATESO WALIYOPATA KUTOKA KWA HITLER NA WAJIRUDI WASIYAFANYE KAMA WALIYOFANYIWA WAO

    MUNGU TUPE NGUVU WALIMWENGU SOTE KUKEMEA MABAYA HAYA

    AMINA

    ReplyDelete
  5. Ubinaadam ndio sehemu ya mhimili mkuu wa Uumini.

    Mungu akuzidishie wewe Nyota C.Ronaldo!

    ReplyDelete
  6. USTAA NI VITENDO NA SIO MATUMIZI MABAYA YA KIFEDHA.

    Mungu akupe zaidi wewe CHRISTIANO RONALDO kwa kutoa fungu la Kipato chako kwa kuwawezesha waliofikwa na masahibu makubwa sana!!!

    ReplyDelete
  7. Mungu ashukuriwe, hiyo ni zaidi ya tsh billion 3.ni bajeti ya wizara kadhaa hapa kwetu.. kutoa ni moyo si utajiri.

    ReplyDelete
  8. Kweli kabisa Palestina si Waislam pekee kuna wakristo pia, nina rafiki ambaye ni mpalestina na ni mkristo mkatoliki so being Arabic does not connote Islamic

    ReplyDelete
  9. Uyahudi ni dini, ila Israel ni nchi ambapo raia wake wengi ni wayahudi, ila kuna waisraeli Wakristo na hata Waislam.

    Ni sawa ni wayahudi ndio walimmua Yesu (kwani mafundisho yake yalipingana na dini yao ya Kiyahudi), ndio maana haisemwi Waisraeli ndio walimuua Yesu.

    Ila ni kweli kwamba Sio Wapelistina wote ni waislamu, ila asilimia kubwa ni waislamu, ni kama ilivyo Zanzibar vile.

    ReplyDelete
  10. Hapo usichanganye mambo ya dini na ubinadamu wa Ronaldo,si kitu cha ajabu kwa yeye kujenga shule gaza baada ya kuona ukatili waliofanyiwa watu wa gaza ambao kuna mchanganyiko wa waislam na wakristo.Kitu ambacho ingebidi ushangae kwanini jumuiya ya kimataifa haijaliona hilo mpaka akatokea yeye peke yake then ndio uanze kufikiria vingine

    ReplyDelete
  11. Mjomba hizi vita haziusiani na dini sio..hamna mtu anayeweza kwenda kuuwa watoto na wanawake kwaajiri ya dini..ni Israel wanaiba hardhi..wanasingizia dini..haziusiani na dini..binadamu wote tupo sawa na siku moja wote tunakufa...

    ReplyDelete
  12. jamani wabongo someni dini mnakuwa wajinga kabisa mkizungumzia mambo ya dini ohhhh yesu mkiristo ohhhhhh mungu hana dini jamani. nakupeni faida kidogo dini maana yake ni mfumo wa maisha. sasa unaposema mungu hana dini unakua unasema nini?

    ReplyDelete
  13. Kuna waisrael na Wa Zion. Wenyeji wa Israel wametawaliwa na Wa Zionist ambao ni waIsrael wa kujipachika kutoka Ulaya wanajiita Ashkenizi Jews.

    Hilo mnatakiwa waTanzania muelewe kama hamuelewi chokonyoweni katika google inakupa historia nzima ya watawala wa Kizion ambao wanatawala Marekani na sehemu za Ulimwengu. Mjarumani (Hitler) aliwatambua siku nyingi na alitahadhaisha lakini analaaniwa kwa kuwaangamiza. Athari ndio zinaonekana leo wanaitawala Israel baada ya kukabidhiwa na Waingereza kipande tu cha Ardhi hao WaZion waliotoka ulaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...