Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania,
Lawrence Mafuru (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa benki
hiyo, Lemweli Shiwakwe katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam
jana, wakati wa uzinduzi
wa kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa
Kuchukua Hatua’ ambayo viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na
kusikiliza mahitaji yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania,
Lawrence Mafuru (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa
benki hiyo, katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana,
wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa
Kuchukua Hatua’ ambayo viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na
kusikiliza mahitaji yao.Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa NBC, Jane
Dogani.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru
(kushoto) akisaidia kuhesabu pesa ili kumhudumia mmoja wa wateja wa
NBC wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru
(katikati) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakati
wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa
Kuchukua Hatua’ ambayo viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na
kusikiliza mahitaji yao.
Benki ya NBC imezindua kampeni ya kuboresha huduma kwa wateja ambayo itaendelea hadi mwisho
wa mwezi Novemba 2012 na kuhusisha uongozi mzima wa NBC. Kampeni hiyo
ijulikanayo kama kama Leadership in action – I CARE, au kwa Kiswahili
"Uongozi kwa kuchukua hatua - NAJALI", inalenga katika kuboresha
utoaji wa huduma kwa wateja NBC. Ni siku ambayo lengo lake kuu ni kwa Uongozi
wa NBC kutoa huduma kwa wateja.
Kampeni
ilizinduliwa katika tawi la NBC Corporate, lililopo jijini Dar es Salaam. Ili
kuzindua rasmi kampeni hii Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Lawrence Mafuru
alikuwa Kiongozi wa kwanza wa benki kwenda tawini kuongea na wateja na kutoa
huduma. Bw Mafuru alizungumza na wateja wa NBC juu ya masuala mbali mbali
ikiwamo pia kuridhika kwao na huduma ya NBC na kama wana mapendekezo yoyote.
"Uongozi
kwa kuchukua hatua – NAJALI” itafanyika kwenye matawi kadhaa ya NBC. Kampeni
hii itakayofanyika kati ya Novemba 19 na 30 2012 itashirikisha jumla ya matawi
25 nchini. Matawi 18 yakiwa jijini Dar es salaam na matawi 7 mengine yakiwa
mkoani.
Kampeni hii ni
sehemu ya Kampeni nyingine ya kibenki inayolenga kurahisisha maisha ya wateja
wake kwa kuwapatia huduma bora zaidi. "Uongozi kwa kuchukua hatua –
NAJALI” inakusudia kuweka wateja wa NBC mbele na kuhakikisha wanaridhika na
huduma zitolewazo na benki hiyo na hatimaye kuwa karibu zaidi na wateja wake.
Ili kuonesha
umuhimu wa wateja katika kufanikisha biashara yao, Uongozi wa NBC umeamua
kutumia nusu siku kutembelea matawi
mbali mbali wakiwa na lengo la kusikiliza maoni ya wateja, malalamiko au hata
sifa nzuri pale benki inapofanya jambo la kuridhisha wateja wake, na pia
kusaidia kwenye zoezi zima la utoaji wa huduma kwa wateja.
Miongoni mwa
masuala yaliyozungumzwa kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Lawrence Mafuru na
wateja ni suala zima la uwizi unaofanyika kwa kutumia mashine za kutolea hela
za ATM ambalo ni tatizo linaloathiri wateja wengi wa mabenki nchini.
Akizungumzia juu ya suala hilo Bw. Mafuru alisema, "Wizi kwa kutumia kadi
za ATM, ni tatizo kubwa kwa mabenki mengi na wateja wao, hasa kwa nchi za Ulaya
Mashariki, ambapo hili tatizo limekithiri. Hizi siku za karibuni tatizo hili
limeongezeka nchini na kusababisha usumbufu mkubwa sana kwa wateja wa mabenki
ya Tanzania". Mr Mafuru Aliongeza, "Asasi ya Mabenki ya Tanzania
inafanya mpango wa kuhakikisha tatizo hili linatokomezwa kabisa nchini ili
kuhakikisha kuwa wateja wetu wote wanalindwa ipasavyo.”
Kati ya masuala mengine waliogusia wateja ni pamoja na mtandao kupungua kwa
spidi mara nyingine, jambo ambalo linasababisha foleni ndefu wakati wateja
wakisubiri kupata huduma. Kuna wateja kadhaa pia ambao walimwaga sifa kwa Bw.
Mafuru kuhusu utendaji wa benki yake, ambapo mteja kutoka kampuni ya Chemi
& Cotex alisifu NBC kwa kuboresha huduma ya TISS, ambayo zamani ilikuwa
ikichukua siku 2-3, ila sasa inakamilika ndani ya siku moja tu.


kwa nini hamtaki kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa maofisini???
ReplyDeleteSafi sana, nimeipenda hii.
ReplyDelete