Mkuu wa Chuo cha
Usafirishaji(NIT), Mhandisi, Dkt. Zacharia Mganilwa(aliyevaa suti ya Kaki), akimuonyesha
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe(Kulia kwa Mkuu wa Chuo), eneo ambalo
Chuo kimelitenga kwa ajili ya wenye Magari watakaomua kupaki magari yao na
kwenda kutumia Usafiri wa Treni inayotoka Ubungo kuelekea Stesheni jijini Dar
es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha
Usafirishaji(NIT), Mhandisi.Dkt. Zacharia Mganilwa(aliyevaa suti ya Kaki), akimueleza
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe(Kulia kwa Mkuu wa Chuo), namna ambavyo
Maktaba ya Chuo hicho inavyofanya kazi, chuoni hapo. Dk Mwamkyembe
alipita katika maeneo mbalimbali kabla ya kuhudhuria mahafali ya 28 ya Chuoni
hapo.
Baadhi ya Wageni walioalikwa
katika mahafali ya 28 ya Chuo cha Usafirishaji(NIT), wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe leo mchana katika Viwanja vya Chuo hicho.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe
akihutubia wahitimu pamoja na Wageni waalikwa katika mahafali ya 28 ya Chuo cha
Usafirishaji(NIT), Mahafali hayo yamefanyika katika Viwanja vya Chuo hicho, ambapo wahitimu wa Kozi mbalimbali wametunukiwa Stashahada za Kawada, Stashahada
za Juu na Shahada.
Waziri wa Uchukuzi.Dk.
Harrison Mwakyembe(Aliyevaa kofia Nyekundu),akiwa katika picha ya pamoja na
Wahitimu wa kozi mbalimbali kutoka
katika Chuo Cha Usafirirshaji(NIT),jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...