Hawa jamaa wa UN wasitake kutuchezea akili. Adhabu ya kifo ni mbaya, sawa; lakini inastahili. Nimepata kumhoji Jaji Samatta juu ya adhabu hiyo. Yeye anaiunga mkono. Hoja yake ni kwamba kuna kesi ukiisikiliza, ukajua namna mhusika alivyoshiriki kumuua binadamu mwenzake, kama kweli ni Jaji mtenda haki, atamhukumu adhabu ya kifo. Juzi hapa wanajeshi wamehukumiwa kifo kwa kumuua Swetu. Hawa watu ukiwakuta mitaani wanavyoadhibu binadamu wengine hadi kuwaua, hakika huwezi kuwaonea huruma nao wanapohukumiwa.
Fikiria, majambazi wanaingia nyumbani kwako na kuiua familia yako, kisha wanaambulia kuchukua sh laki moja, au kuku, au mbuzi. Katika mazingira kama hayo, wahusika wakipatikana hakuna adhabu sahihi kwao zaidi ya kunyongwa, tena si kunyongwa tu, bali kunyongwa hadi kufa.
Kama kweli UN wanaona adhabu hii haifai, basi waanze na wafadhili wao wakuu, "mabwana" wa demokrasia-Marekani ili nao waache kufanya hivyo. Saddam Husseina alinyongwa, Gaddafi kauawa na wakala wao Wamarekani na Wafaransa; iweje kuwaua hawa iwe halali, lakini sisi kuwanyonga wanaowanyonga ndugu zetu iwe si haki?
Afrika Kusini walijipendekeza kufuta adhabu hiyo kwa busara zas Jaji Mwalusanya wa Tanzania. Sasa wanajuta! Wanataka adhabu ya kifo irejeshwe maana ushenzi umepindukia nchini humo.
Ituache kuimba wimbo wa UN pamoja na asasi za kiraia ambazo kazi yake ni kusaka fedha. Adhabu ya kifo inawafaa sana wale wanaoistahili. Haki ya kuishi isiwe kwa muuaji tu, bali tutazame na yule aliyeuawa anatendewa haki vipi!
Mdau Manyerere
Nawasilisha

Tena wanastahili kuwekwa uwanja wa mpira wa miguu na wananchi ndio tuwapige kwa mawe madogomadogo hadi wafe kwa MATESO MAKALI! NINA UCHUNGU NA WATU WA NAMNA HIII WE ACHA TU MANYERERE.
ReplyDelete%#@!%^&)(*&^% WAKUBWA
NDIO TATIZO SHERIA ZA NCHI AU DINI ZIMEZIDIWA NA BRITISH LAW NCHINI TANZANIA. KUMBUKA HAO WANAJESHI WAMEZULUMU UHAI WA MTU.
ReplyDelete
ReplyDeleteHii UN ya kuiangalia sana hii.