Kwanza kabisa napenda kutoa shukurani zangu
kwa wizara sabab shule zimeongezeka na hasa kwa vijijini na mijini hii imefanya
jamii ya watanzania wengi kwenda shule hata kama ajafanya vizuri kwenye masomo
lakini wamejifunza kuishi na watu na mambo mengi iliyoko kwenye jamii.
Kusudi langu kubwa hasa ni, Kuhusu mitihani
ya Taifa kweli hasa kuanzia ile mitihani ya kidato cha 4 na cha 6. Oja yangu ni
kuhusu mtu anapoumwa ghafla akalazwa au mwingine akachanganyikiwa na hawezi
kabisa kufanya mtihani akashindwa kutokana na hali yanayokuwa nayo kwa wakati
ule.
Mimi kama mwanajamii na mzazi nilikuwa naomba kipengele kinachosema hata
kama mwanafunzi anaumwa afanye mtihani naomba kibadilishwe. Iwe endapo
mwanafunzi ameumwa gafula na daktari akathibitisha, naomba asifanye mtihani bali ahirishe na afanye mwaka unaokuja kuliko kufanya wakati yuko kwenye hali mbaya na matokeo
yakaja ameshindwa na wakati hajaumwa alikuwa na maendeleo ya kuweza kufanya
vizuri alikuwa nao.
Naomba Wizara kushirikiana na Baraza la Mitihani la Taifa waliangalie hili manaake mtoto amesoma miaka 4 au 6 inapofikia hatua kwa
bahati mbaya akaumwa gafula na jinsi karo inavyoumiza katika masomo tunaomba
wabadilishe hiyo sheria make mambo yakusema afanye matokeo yakitoka vibaya
arudie kama mtahiniwa wa kujitegemea naona hiyo haiamsaidi mwanafunzi kama huyo.
Naomba kuwasilisha
MDAU WA ELIMU


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...