Mgonjwa Stella Samuel Mwita mwenye umri wa miaka 32 amefariki dunia Novemba 2, 2012 saa 12 asubuhi katika Idara ya Magonjwa ya Akili Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa toka Septemba 2012.
Stella alikuja Dar es Salaam kutokea Mtwara miaka mingi iliyopita na wakati wa ugonjwa wake hakupata kutembelewa na ndugu yeyote yule.
Shughuli za mazishi zinasubiri ndugu wa marehemu. Mungu ailaze roho yake pema peponi.
|
Imetoloewa na;
Aminiel Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Hospitali ya Taifa Muhimbili




Michuzi sasa watu watamtambuaje huyu mtu ikiwa picha umeficha?
ReplyDelete