Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia taarifa kuhusu wanajeshi kupiga askari wa usalama barabarani. Sababu ambazo zimekuwa zikitolewa mara nyingi ni askari wa usalama Barabarani kuchelewesha kuruhusu magari, (hususan upande ambao wanajeshi hao wapo). 

Binafsi, nilikuwa nikisikitishwa sana na taarifa hizo za kupigwa kwa Askari wa usalama barabarani kutokana na sababu kuu mbili. Kwanza, Askari wa Usalama Barabarani na Wanajeshi wote ni watumishi wa Serikali na pia wawakilishi wa vyombo vya usalama. 

Hivyo, katika mazingira ya kawaida kabisa hakuna mtu mwenye busara anaweza kuona makundi hayo yakipambana. Pili, niliamini kuwa kucheleweshwa kuruhusu magari sio kosa la askari wa usalama barabarani bali ni kutokana na mazingira ya miundombinu yetu. 

 Hata hivyo, jana asubuhi tarehe 28 Novemba 2012, nilipata mawazo mapya. Wakati mwingine askari wa usalama Barabarani wanasababisha foleni isiyokuwa na msingi, na pengine ndiyo sababu wanajeshi wanaamua kuchukua uamuzi wa kuwapiga. 

Kwa mfano, jana asubuhi bila sababu za msingi, askari aliyekuwa kwenye taa za St. Peter (mbele ya kituo Mbuyuni) alisababisha foleni isiyokuwa ya msingi, kwa maoni yangu.

 Askari huyu, alisimamisha gari zilizokuwa zinatoka barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwa takribani dk. 40 kuanzia saa 12:55 hadi saa 1:35 bila sababu za msingi huku barabara kuanzia kwenye taa za St. Peter kuelekea mjini ikiwa nyeupe. 

Naamini alifanya hivyo ili kutoa nafasi kwa msafara wa kiongozi kupita. Lakini, tatizo langu na askari huyu ni kwamba alikuwa na redio ya mawasiliano (na ninasikia kuwa wanapewa hela ya vocha kwa simu zao za mikononi) sasa iweje askari huyu azuie magari kwa dk. 40 kusubiri msafara? 

Kwanini alishindwa kuziruhusu gari ziende na msafara ukiwa utayari ndipo azuie? 

 Jibu langu ni moja tu, askari huyu hata kama ni mtaalam na amefuzu vizuri sana mafunzo ya uaskari,HAFAI KUWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI. HIVYO, NAOMBA KAMANDA MPINGA AMUONDOE NA APEWE JUKUMU JINGINE.

MDAU WA GLOBU YA JAMII

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kamanda Mpinga hawezi kumuadhibu kwasababu hayo aliyoyafanya huyo traffic ni maagizo kutoka kwake, infwact umemufwagilia aongezwe cheo!!

    ReplyDelete
  2. Bwana Michuzi, ni Tanzania tu ambako trafiki wanadhani wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi (more efficiently) kushinda taa za kuongozea magari. Ni jambo la ajabu sana kuona askari wanang'ang'ania kuongoza magari sehemu zenye taa zilizowekwa kwa ajili hiyo. Matokeo yake ni kusababisha hali kuwa mbaya zaidi barabarani. Ukiona foleni ya magari ni ndefu sana na haisogei basi ujue mbele kuna trafiki amejipa kazi ya kuongoza magari pamoja na kuwepo taa zinazofanya kazi. Cha kushangaza ni kwamba askari hawa wanaojifanya wachapa kazi huwa hawakai sehemu sehemu zenye msongamano wa magari lakini zisizokuwa na taa, kwa mfano makutano ya barabara za Mandela na Kilwa jijini Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na wewe,lakini kwa upande mwingine wa shilingi, taa za kuongoza magari zikiwa hazifanyi kazi ni hawa hawa wanausalama wa barabarani wanaokaa hapo kwenye makutano(hadi usiku) kukufanya upite salama bila ajali na kuwahi huko uendekako(Wanastahili pongezi!).Nao ni binadamu,kwa hiyo tuwavumilile siyo kuwapiga na kuwatukana,baada ya muda si mrefu tatizo la foleni litakuwa historia.

    David V

    ReplyDelete
  4. Siyo kosa lake, hata kama yuko na radio na vocha kwenye simu, je kama kapewa AMRI ayasimamishe magari?

    Nionavyo mimi ni mfumo mzima wa kufunga na kuzuia magari kukiwa na misafara uangaliwe upya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana hii inatokana na mfumo mbovu wa kujipa madaraka kwamba yy ndo final say. rushwa adui wa haki. unahonga ili upewe kofia ya traffik wkt hujui kazi

      Delete
  5. labda nijaribu kumtetea kidogo huyo traffick: Inapofika hiyo mida ya asb nhiyo njia ya kwenda mjini kuanzia hapo st. peter inafunga na magari hayaendi kabisa huko mjini. hivyo trafik hawezi kuruhusu mnagari sababu mjini hayaendi na wala sio lazma iwe amewazuia tu. kama ni viongozi wewe muda wote huo ulisikia ving'ora? hebu chunguza tena hilo jambo, hiyo mida kipanfde hicho ni balaa!

    ReplyDelete
  6. Mimi nawalaumu hao viongozi wanaoandaliwa barabara isiwe na foleni kwao..waachwe nao waonje joto la foleni ili waboreshe mfumo mzima wa usafiri(barabara)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...