Mkurugenzi wa Kampuni Mpya ya QS Muhonda J Entertainment, Joseph Muhonga
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
wakati akitangaza uzinduzi wa Kampuni yake hiyo na Kutangaza ujio wa
Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo,JB Mpiana ambaye
atatumbuiza katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam Novemba
30.Katika onyesho hilo ambalo litasindikizwa na wanamuziki mbali mbali
hapa nchini wakiwemo,H-Baba,MB Dog na Ney wa Mitego ambao wapo chini ya
lebo ya Kampuni hiyo pia kutafanyika uzinduzi rasmi wa Albamu mpya ya
Bendi ya Mashujaa uitwao "Risasi Kidole".Wengine pichani ni Mratibu wa Onyesho hilo,King Dodoo (katikati) na Meneja wa Bendi ya Mashujaa,Martin Sospeter.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Hamis Ramadhan a.k.a H-Baba (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo juu ya maandalizi yake ya kufanya shoo jukwaa moja na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo,JB Mpiana ambaye
atatumbuiza katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam Novemba 30.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...