Mshambuliaji wa timu ya Kilimajaro Stars, Simon Msuva (12) akichanja mbuga baada ya kumtoka beki wa
timu ya Sudani, Faris Abdallah wakati wa mchezo wa michuano ya
Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela Jijini Kampala,Uganda leo.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.
Erasto Nyoni wa Kilimanjaro Stars (4) na beki wa timu ya Sudan, Faris
Abdallah wakiwania mpira wakati wa mchezo wa michuano ya Chalenge
uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala,Uganda.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngassa akikokota
mpira uliozaa goli pili wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge 2012
dhidi ya Sudan uliochezwa katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala leo.
Kilimanjaro Stars wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na John
Bocco wakati wa mchezo dhidi ya Sudan katika michuano ya CECAFA
Challenge katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala.
Mashabiki wa timu ya Kilimanjaro Stars waliosafiri kutoka mkoani
Kagera wakishangilia baada ya kufungwa kwa goli la kwanza wakati wa
mchezo wa Cecafa Challenge 2012 dhidi ya Sudan uliochezwa katika
Uwanja wa Mandela Jijini Kampala leo.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.


Tanzania kuna vipaji ambavyo vinahitaji kuendelezwa na TFF wakiwa na mpangilio mzuri kuanzia mashuleni ,vilabuni hadi ngazi ya uteuzi wa wachezaji na makocha wanaofundisha taifa stars ,kutakuwa na mafanikio makubwa ktk soka ngazi ya kimataifa.Big up ,mdau ughaibuni
ReplyDeleteHii inafaa iwe picha ya mwaka. Naona kushoto Mzenji meno 32 nje kwa furaha akiishangilia Bara. Safi sana namna hii! - Kilakshari, USA
ReplyDeleteNi mwelekeo mzuri na timu ilikuwa na vijana wengi. Inabidi tuongeze vijana zaidi ktk timu ili baada ya miaka 2 timu yote isiwe na mchezaji aliye zaidi ya miaka 25.
ReplyDeleteMwelekeo mzuri,safi sana vijana,Jumatano `man to watch'= Didier Kavumbagu ,apewe ulinzi maalum.
ReplyDeleteMashabiki kutoka mkoani Kagera-'Mwakola muno!!!'endeleeni kuwashangilia vijana warudi na kombe
David V
hiyo fulana tu haijalishi kama yeye ni mzenji hapo anawakilisha TZ tu,hakuna kingine
ReplyDeleteKwa taarifa, Kavumbagu hayupo ktk timu ya Burundi. Kocha anasema amechukua wachezaji wanaocheza ligi ya Burundi tu.
ReplyDelete