Mshambuliaji wa timu ya Kilimajaro Stars, Simon Msuva (12) akichanja mbuga baada ya kumtoka beki wa timu ya Sudani, Faris Abdallah wakati wa mchezo wa michuano ya Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela Jijini Kampala,Uganda leo.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.
Erasto Nyoni wa Kilimanjaro Stars (4) na beki wa timu ya Sudan, Faris Abdallah wakiwania mpira wakati wa mchezo wa michuano ya Chalenge uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala,Uganda.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngassa akikokota mpira uliozaa goli pili wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge 2012 dhidi ya Sudan uliochezwa katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala  leo.
Kilimanjaro Stars wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na John Bocco wakati wa mchezo dhidi ya Sudan katika michuano ya CECAFA Challenge katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala.
Mashabiki wa timu ya Kilimanjaro Stars waliosafiri kutoka mkoani Kagera wakishangilia baada ya kufungwa kwa goli la kwanza wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge 2012 dhidi ya Sudan uliochezwa katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala leo.Kilimajaro Stars imeshinda bao 2-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tanzania kuna vipaji ambavyo vinahitaji kuendelezwa na TFF wakiwa na mpangilio mzuri kuanzia mashuleni ,vilabuni hadi ngazi ya uteuzi wa wachezaji na makocha wanaofundisha taifa stars ,kutakuwa na mafanikio makubwa ktk soka ngazi ya kimataifa.Big up ,mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Hii inafaa iwe picha ya mwaka. Naona kushoto Mzenji meno 32 nje kwa furaha akiishangilia Bara. Safi sana namna hii! - Kilakshari, USA

    ReplyDelete
  3. Ni mwelekeo mzuri na timu ilikuwa na vijana wengi. Inabidi tuongeze vijana zaidi ktk timu ili baada ya miaka 2 timu yote isiwe na mchezaji aliye zaidi ya miaka 25.

    ReplyDelete
  4. Mwelekeo mzuri,safi sana vijana,Jumatano `man to watch'= Didier Kavumbagu ,apewe ulinzi maalum.

    Mashabiki kutoka mkoani Kagera-'Mwakola muno!!!'endeleeni kuwashangilia vijana warudi na kombe

    David V

    ReplyDelete
  5. hiyo fulana tu haijalishi kama yeye ni mzenji hapo anawakilisha TZ tu,hakuna kingine

    ReplyDelete
  6. Kwa taarifa, Kavumbagu hayupo ktk timu ya Burundi. Kocha anasema amechukua wachezaji wanaocheza ligi ya Burundi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...