Mkurugenzi wa Shirika la kazi nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo akitoa hotuba yake siku ya kufunga maonesho ya wajasiria mali MOWE 2012 yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Malawi nchini Tanzania Bi. Flossie Gomile Chidyaonga akitoa hotuba yake kwa wajasiria mali wa MOWE 2012.
Msichana Mjasiriamali akipokea cheti cha ushiriki wa MOWE 2012 toka kwa Balozi wa Malawi Bi. Flossie Gomile Chidyaonga (kushoto). Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi ya MOWE Bi. Elihaika Mrema.
Mkurugenzi wa ILO nchini Bw. Alexio Musindo (kulia) na Bi. Teddy Rucho wakipokea cheti cha ushiriki toka kwa balozi wa Malawi katika sherehe za ufungaji wa maonyesho ya wajasiriamali MOWE 2012.
Balozi wa Malawi Tanzania Bi. Flossie Gomile Chidyaonga (kushoto), Mkurugenzi wa ILO nchini Bw. Alexio Musindo sambamba na Mwenyekiti wa MOWE Bi. Elihaika Mrema (katikati) wakiangalia bidhaa zitokanazo na Mti wa Mbuyu wakati wa sherehe za ufungaji wa maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali MOWE 2012 yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Balozi akitembea banda la ILO katika maonyesho ya MOWE 2012.
Balozi wa Malawi akipata maelezo toka kwa team ya ILO walioandaa maonyesho ya MOWE kwa kushirikiana na Taasisi ya WAMA.
Balozi wa Malawi na Mkurugenzi wa ILO nchini wakinunua mifuko maalumu ya kuhifazia Laptops na iPad iliyotengenezwa kwa ubunifu mkubwa kwa kutumia malighafi ya Tanzania Kitenge toka kwa Mwanamke Mjasiria mali wa MOWE 2012 katika maonyesho hayo.
Bwana Pius Mikongoti wa GS1 akitoa Mada kuhusu Barcode kwa washiriki wa MOWE 2012.
Picha ya Pamoja Kamati ya MOWE na wageni rasmi siku ya kufunga maonesho ya MOWE 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...