Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akifungua mkutano wa Taasisi ya Maendeleo ya Kiuchumi na Mipango ya Afrika- IDEP. Tanzania ni
mjumbe wa Bodi ya Magavana katika taasisi hii ambayo hujishughulisha na utoaji
wa mafunzo ya kitaalam kwa wataalam wa serikali za nchi za Kiafrika.
Wajumbe
wengine katika Bodi ya Magavana ni pamoja na Misri, Kenya, Nijeria na
Zimbambwe. IDEPambayo makao yake makuu yapo nchini Senegal ni moja ya Taasisi
za Umoja wa Mataifa na inatimiza miaka
50 tangu kuanzishwa kwake.
Hivyo, kupitia IDEP watanzania wanaweza wakanufaika
na program mbalimbali za mafunzo zinazotolewa au kudhaminiwa na taasisi hii.
Kwa taarifa zaidi tembelea katika website ya IDEP: http://www.unidep.org/ .Kozi za kipaumbele zinazotolewa au kuratibiwa na
IDEP ni masuala ya kiuchumi, Mipango, Maendeleo ya Nishati ya gesi, uranium na
masuala ya usimamizi wa mikataba
Prof. Humphrey Mushi Kushoto na Prof. Mutahaba wa USDM
wakifutatilia mijadala pamoja na wataalam wengine.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akiongea na wanahabari wa Senegal
1. Mhe.
Naibu waziri (katikati) akibadilishana mawazo na Prof. Mushi kulia na Prof. Mutahaba (kushoto) wakati wa mapumziko ya mkutano huo mjini
Dakar, Senegal. Picha na Thomas M.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...