Leo Tarehe 21.11.2012 imetimia miaka miwili (2) tangu utuache hapa Duniani Mama Mary Mwingira. Maisha yetu sisi wanao, mama yako, wakwe , wajukuu, wadogo,wifi, wapwa, majirani, ndugu na marafiki zako wote yamebadilika na  si kama ulivyokuwa nasi. 

Tunakukumbuka na kuukosa upendo, ucheshi na uchapakazi na moyo wa kutokata tamaa uliokuwa nao. Umekuwa chachu ya maisha yetu na msaada mkubwa kwetu sote. Mungu alikuongoza kwa yote hadi   kukujalia kifo chema ukiwa katika imani thabiti. 

Mapenzi yake MUNGU  Baba yatizwe kwani ndiye aliyetupa zawadi ya wewe kuwa mwanetu, mama yetu, bibi, dada, shangazi, mkwe, wifi  shemeji, rafiki na jirani yetu mpendwa. Tunaahidi kuendelea kukuenzi daima kwa somo kuu lako la upendo usio na masharti.

Ulale salama mama yetu! Nasi tunakuombea kwa Mungu akupokee mbinguni ambako tunaamini umefika. Uendelee kutuombea sisi wanao na ndugu wote ulituacha hapa duniani.Tunakupenda sana mama na kamwe hatutasahau mapenzi yako kwetu.
Machozi ni mengi machoni mwetu na hayapimiki kamwe.

Tunashukuru kwa mafunzo ambayo yamezaa baraka na mafanikio tele. Ulikuwa hupendi kuona tunasononeka na tunaamini hadi sasa hupendi kutuona tukisoneneka hivyo tunasherehekea maisha yako matakatifu na tunasema, Asante MUNGU kwa zawadi hii kubwa ya kuwa watoto  na ndugu zako..Umetuonyesha mfano wa kuigwa nasi wamama,wanawake na watu  wengine wote mama Mwingira..

Tunakupenda na kuta kuenzi daima Milele na milele!!!

Kutakuwa na Misa za kumuombea Mama Mary Mwinngira katika  kanisa kuu la Mtakatifu Joseph’s  tarehe 21 /11/2012 . Ratiba ni kama ifuatavyo: Saa 12 .45 asubuhi, Saa 7 mchana na jioni ya 11 jioni. Pia Bethania House-Upanga saa 6:30 asubuhi Siku hiyo hiyo. 

Misa hizi zitaendelea kwa wiki hii yote yani tar 22 - 25 Novemba katika makanisa hayo na kila Jumapili St Gasper, Kunduchi misa ya 2(saa 1 kamili asubuhi).KARIBUNI SANA!!


Raha ya milele Umpe Eee Bwana,na Mwanga milele Umuangazie...Mary John Mwingira astarehe  kwa AMANI..

AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Rest in peace mum,am relieved i have seen your picture,its bitter sweet feelings for me....i just wish you were here and see the woman i become.... am sure you have been my guardian angel,i will keep you in prayers and close to my heart....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...