Sheikh Farid Kabla ya kunyolewa ndevu.
VIONGOZI wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikhe Faridi Hadi Ahmed na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh Mselem Ali Mselem, wamewasilisha maombi Mahakama Kuu ya Vuga Zanzibar, kutaka kufungua kesi kupinga kunyolewa ndevu wakiwa mahabusu.
Kutokana na ombi hilo, Mahakama Kuu ya Vuga mjini hapa, imekubali ombi hilo na kutoa uamuzi wa kuwaruhusu viongozi hao, wafungue kesi ya madai, kupinga kunyolewa ndevu zao na kutotendewa haki wakiwa mahabusu. Sheikh Farid na wenzake, wanashtakiwa kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa taifa. 
Uamuzi wa kuwaruhusu viongozi hao wafungue kesi ya madai, umetolewa  na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi, baada ya kupitia kwa makini maombi ya watuhumiwa hao. 
Washtakiwa hao waliwasilisha mambo hayo Novemba 8, mwaka huu, kupitia kwa mawakili wao, wakipinga kitendo cha polisi kuwanyoa ndevu na kutowatendea haki wakiwa mahabusu. 
Maombi hayo yaliwasilishwa na washtakiwa wanane, akiwemo Sheikh Farid na Mwenyekiti wa Uamsho, Sheikh Mselem. Wengine katika kesi hiyo ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar. 
Akitoa uamuzi wa kufungua kesi ya kupinga kunyolewa ndevu, Jaji Kazi alisema watuhumiwa wana haki ya kufungua kesi mahakama kuu juu ya kile wanachokilalamikia na kwamba Mahakama kuu itakuwa na uamuzi wa kuyasikiliza madai yao tofauti na kesi ya msingi ya uchochezi na kuhatarisha amani. 
Kupitia kwa mawakili wao, watuhumiwa hao walidai kuwa wananyimwa uhuru na haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku kufuga ndevu wakiwa rumande ya Chuo cha Mafunzo (Magereza).
Katika kesi yao ya msingi, watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya kutoa lugha za uchochezi, kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara mjini Zanzibar. 
Wakizungumzia kesi ya msingi kwa watuhumiwa hao, waendesha mashtaka wa serikali walidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamili na kwamba wanaomba siku nyingine ya kutajwa. 
Sheikh Farid baada ya kunyolewa ndevu.
Mrajis huyo wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 29, itakapotajwa tena.
Kama kawaida, Jeshi la Polisi lilifunga barabara zote za kuingia na kutoka mahakamani na kuimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama hiyo ambapo kila pembe walionekana makachero wa polisi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wenye silaha za moto. 
Baadhi ya wananchi waliofika mahakamani hapo, waliwataka waandishi wa habari kuandika ukweli kuhusiana na kesi hiyo ili kuinusuru nchi na machafuko. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Sasa Sh Soraga aliyemwagiwa tindikali yeye atafungua kesi wapi?

    ReplyDelete
  2. Utata mtupu kwani ndevu ni issue ama itatumika kuziba issue ya msingi!!wangapi wamenyolewa wakiingia humo!! Nisheria kiafya ama kiusalama ama vyote!! Hebu wajuaji mtujuze!! ndevundevu...! Ah..

    ReplyDelete
  3. kwanza kapendeza kuliko alivyokuwa nazo aendeleee kuzinyoa.

    ReplyDelete
  4. Huyu mzee kavu kweli,cheki alivyoendeza baada ya kukatwa ndevu zake,anaonekana mtanashati kabisa,cheki hyo picha ya juu alivyokuwa na ndevu anavyoonekana ruff utazania mzee wa miaka 78.hahha!! Ndevu hazikutoi sheikh,zinakutia uzee tu..

    ReplyDelete
  5. Mashallahu Sheikh Farid anapendeza iwe ana ndevu au bila ndevu.

    ReplyDelete
  6. Kunyolewa ngevu imekuwa ishu kwanini, huyu bwana aliyenyolewa haoni kwamba amependeza baada ya kunyolewa, amekuwa more handsome kuliko alipo kuwa na mandevu yake.

    ReplyDelete


  7. Mbona baada ya kunyoa amependeza sana hata kuliko akiwa na ndevu
    bwana mzee acha hzi mambo bwana yaani hapo ndo naona umependeza haswa tena haswa kama African King vile

    ReplyDelete
  8. Hoja hapa sio kupendeza, hoja ni kufanyiwa kitu bila matakwa yake akiwa mahabusu. Elewa kwamba bado hajawa mfungwa kwa hiyo anastahili haki kama raia wa kawaida.

    ReplyDelete
  9. Asiyejua ndevu ni nini na zina maana gani lazima atasema yanayosemwa hapa! labda niwakumbushe mambo mawili:
    1)kisheria
    hivi mahabusu anatakiwa afanyiwe nini akiwa kama mtuhumiwa tu,je,kisheria inaruhusiwa kunyolewa sio ndevu tu bali hata nywele!!?...je ukimnyoa halafu ikabainika hakuwa muhalifu au akashinda kesi na akadai arudishiwe nywele au ndevu zake nani ataweza!!!
    halafu si kunya ndevu tu kuna(kesi ya benki kuu) muheshimiwa alikuwa akitinga mahakamani kwa suti kali kwa kuwa alikuwa mtuhumiwa tu huwezi kuzuia kuvaa vizuri kwa kuwa sheria za kimagereza(chuo cha mafunzo) bado hazija mbana bado kwa kuwa ni mtuhumiwa tu sasa iweje hawa uamsho hata kubadilishwa nguo iwe hairuhusiwi!!??
    2)kiimani
    historia inatuonyesha kwamba mitume na manabii wote walifuga ndevu na mitume hawafanyi mambo ila kwa amri ya mola wao aliye watuma hata wasio waislamu tukiangalia filamu zemu za yesu, yesu alikuwa na ndevu,daudi alikuwa na ndevu, mussa(moses) alikuwa na ndevu,ibrahimu(abrahamu) alikuwa na ndevu, yusufu(yosefu) alikuwa na ndevu,nuhu alikuwa na andevu na wengi wote walikuwa na ndevu kwa ushahidi wa hizi filamutu kabla ya kuingia kwenye maandiko!!! sasa iweje uamsho iwe ni balaa na kubezwa kwa kufuga ndevu!!?? au hamkuzingatia chochote katika filamu hizo!!??
    "jazba ikizidi,umakini wa kulitenda au kuliendea jambo unapungua"
    ukiwabeza uamsho jua pia umewabeza na mitume yote ya mungu kwa imani yoyote utakayo kuwa nayo alimuradi unaamini tu kuwa mungu alituma mitume!!

    ReplyDelete
  10. KUNYOLEWA NDEVU:

    Imejulikana ya kuwa ni wazi Harakati zenu ni za Kisiasa na sio za ki-Dini ndio maana mmenyolewa ndevu!

    ReplyDelete
  11. Kwa kuwa mpo Kisiasa na sio Kidini,

    Mjiandae na Kanzu mtavuliwa na hizo kofia za vibandiko mkapewa Magwanda ya CUF na Kapelo au makofia ya Mzunguko ya Mapama!!!

    ReplyDelete
  12. Kwa hiyo walitaka waingie mahabusu na mandevu? Jamani tusiendekeze uchafu

    ReplyDelete
  13. ndevu sio uchafu bali ni usafi faridi fuga ndevu mimi pia nnazo ndio maana ukiniona kwa mbaliiiiii unajua yule ni mwanamume.mhhh lakini wewe nikikuona kwa mbali sijui ni mke au mume.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...