Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Lemweli Shiwakwe katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi
wa kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa Kuchukua Hatua’ ambayo viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na kusikiliza mahitaji yao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo, katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa Kuchukua Hatua’ ambayo viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na kusikiliza mahitaji yao.Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa NBC, Jane Dogani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (kushoto) akisaidia kuhesabu pesa ili kumhudumia mmoja wa wateja wa NBC wakati wa uzinduzi huo.


Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya NBC iitwayo ‘Uongozi kwa Kuchukua Hatua’ ambayo viongozi wa juu wa NBC kutembelea wateja na kusikiliza mahitaji yao.

Benki ya NBC imezindua kampeni ya kuboresha huduma kwa wateja ambayo itaendelea hadi mwisho wa mwezi Novemba 2012 na kuhusisha uongozi mzima wa NBC. Kampeni hiyo ijulikanayo kama kama Leadership in action – I CARE, au kwa Kiswahili "Uongozi kwa kuchukua hatua - NAJALI", inalenga katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja NBC. Ni siku ambayo lengo lake kuu ni kwa Uongozi wa NBC kutoa huduma kwa wateja.

Kampeni ilizinduliwa katika tawi la NBC Corporate, lililopo jijini Dar es Salaam. Ili kuzindua rasmi kampeni hii Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Lawrence Mafuru alikuwa Kiongozi wa kwanza wa benki kwenda tawini kuongea na wateja na kutoa huduma. Bw Mafuru alizungumza na wateja wa NBC juu ya masuala mbali mbali ikiwamo pia kuridhika kwao na huduma ya NBC na kama wana mapendekezo yoyote.

"Uongozi kwa kuchukua hatua – NAJALI” itafanyika kwenye matawi kadhaa ya NBC. Kampeni hii itakayofanyika kati ya Novemba 19 na 30 2012 itashirikisha jumla ya matawi 25 nchini. Matawi 18 yakiwa jijini Dar es salaam na matawi 7 mengine yakiwa mkoani.

Kampeni hii ni sehemu ya Kampeni nyingine ya kibenki inayolenga kurahisisha maisha ya wateja wake kwa kuwapatia huduma bora zaidi. "Uongozi kwa kuchukua hatua – NAJALI” inakusudia kuweka wateja wa NBC mbele na kuhakikisha wanaridhika na huduma zitolewazo na benki hiyo na hatimaye kuwa karibu zaidi na wateja wake.

Ili kuonesha umuhimu wa wateja katika kufanikisha biashara yao, Uongozi wa NBC umeamua kutumia nusu siku kutembelea  matawi mbali mbali wakiwa na lengo la kusikiliza maoni ya wateja, malalamiko au hata sifa nzuri pale benki inapofanya jambo la kuridhisha wateja wake, na pia kusaidia kwenye zoezi zima la utoaji wa huduma kwa wateja.

Miongoni mwa masuala yaliyozungumzwa kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Lawrence Mafuru na wateja ni suala zima la uwizi unaofanyika kwa kutumia mashine za kutolea hela za ATM ambalo ni tatizo linaloathiri wateja wengi wa mabenki nchini. Akizungumzia juu ya suala hilo Bw. Mafuru alisema, "Wizi kwa kutumia kadi za ATM, ni tatizo kubwa kwa mabenki mengi na wateja wao, hasa kwa nchi za Ulaya Mashariki, ambapo hili tatizo limekithiri. Hizi siku za karibuni tatizo hili limeongezeka nchini na kusababisha usumbufu mkubwa sana kwa wateja wa mabenki ya Tanzania". Mr Mafuru Aliongeza, "Asasi ya Mabenki ya Tanzania inafanya mpango wa kuhakikisha tatizo hili linatokomezwa kabisa nchini ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wote wanalindwa ipasavyo.”

Kati ya masuala mengine waliogusia wateja ni pamoja na mtandao kupungua kwa spidi mara nyingine, jambo ambalo linasababisha foleni ndefu wakati wateja wakisubiri kupata huduma. Kuna wateja kadhaa pia ambao walimwaga sifa kwa Bw. Mafuru kuhusu utendaji wa benki yake, ambapo mteja kutoka kampuni ya Chemi & Cotex alisifu NBC kwa kuboresha huduma ya TISS, ambayo zamani ilikuwa ikichukua siku 2-3, ila sasa inakamilika ndani ya siku moja tu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kwa nini hamtaki kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa maofisini???

    ReplyDelete
  2. Safi sana, nimeipenda hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...