Leo jiji la Dar es salaam limegubikwa na wingu tokea asubuhi, lakini hii haimzuii Ankal kutukumbusha enzi za Osibisa na wimbo wao wa chacha wa Sunshine Day. Osibisa, iliyoundwa mwaka 1969 jijini London na wana Diaspora wanne toka Ghana, na watatu kutoka Carribean, ilitamba sana enzi hizo za miaka ya 70
Wengi walijifunza kucheza chacha kwa ngoma hii wanamuziki waanzilishi wakiwa Teddy Osei (saxophone,flute, na kuimba), Mac Tontoh (trumpet na kuimba viitikio), Sol Amarfio (drums na kuimba), wote wakiwa wametoka Ghana, Loughty Lassisi Amao (congas, percussion, na midomo ya bata), ftoka Nigeria, Robert Bailey (keyboards), toka Trinidad, Spartacus R (bass), toka Grenada, na Wendell Richardson (gitaa la kwanza na kuimba)


Ankal umetukumbusha mbaaaali!!!
ReplyDelete1975/1976 Secondary za Dar wakati tunakwenda kulima RUVU sekondari, Tunakaa Kibaha, Na kuna bwana mdogo mmoja alikuwa anacheza chacha sana kutoka forodhani. Sijui kama kuna jamaa wanakumbuka enzi hizo.
Ewe Bwaaana usinijuuee nenda kwanza ka... (naogopa kumalizia) haha umenikumbusha mbaali Michu
ReplyDeleteEnzi zile John Kitime alikua bado kijijini na kuja jijini Dar ilikua issue yaani kwa John Kitime alikua akisikia habari za jiji la Dar...
ReplyDelete