MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. (pichani) anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwezi ujao katika klabu ya Simba SC na hadi sasa mustakabali wake haueleweki kama ataongezewa mkataba au la.
Kumekuwa na mawazo tofauti ndani ya Simba SC kuhusu Sunzu, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Tanzania, Sh Milioni 5, kwamba hachezi kwa kiwango cha fedha anazolipwa.
Lakini wengine wanaamini Sunzu anawajibika vizuri na anastahili kwa fedha anayolipwa. Pamoja na hayo, hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo kwa sasa, inatia shaka kama itaweza kuurudia mkataba ule ule wa Sunzu.
Kwa kawaida, baada ya kumaliza mkataba, Simba ili kuendelea kuishi na Sunzu, italazimika kumpa fedha ya dau la usajili, ambalo kwa mwaka haliwezi kuwa chini ya dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. Milioni 20 za Tanzania) na kukubaliana kuhusu mshahara uwe ule ule au mpya.
Kulingana na zengwe lililotawala juu ya dola za Kimarekani 3,500 anazolipwa Sunzu kuna uwezekano Simba ikataka kuuteremsha mshahara huo, hasa ikizingatiwa kuwa, kwa sasa hakuna taarifa zozote za Mzambia huyo kutakiwa na timu, iwe ndani ua nje ya nchi.
Kumalizika kwa mkataba wa Sunzu ni mtihani mwingine kwa Simba, ambayo kwa sasa inakabiliwa na kasheshe la kuingia mkataba mpya na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi ambaye yuko vizuri kisoka na anatolewa macho na Azam na Yanga.
Na suala la usajili linazidi kuwa zito kwa sababu Kamati ya Utendaji ya Simba SC wiki hii imevunja Kamati zote ndogondogo, ikiwemo Kamati ya Usajili, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Zacharia Hans Poppe.



Simba SC haya chacha!!!
ReplyDeletePitisheni 'Kofia' ili kuchangisha si mnajifanya Wajanja wakati fedha hamnazo?
Msimbazi mabahili sana yaani mpaka Mkataba unaanguka chini tarehe zake ninyi mngali mpo usingizini?
ReplyDeleteAma kweli shida haina adabu!
ReplyDeleteMsimbazi matatizo lukuki Klabuni, Migogoro kibao makundi hayaelewani, kila kukicha Maandamano ya Mapinduzi Klabuni,,,leo tena Mkataba wa Mchezaji umekwisha huku Akaunti ya Klabu hati hati huenda hata LAKI MOJA haina!
...Inawezekana kwenye Akaunti imebaki hela ya Kitabu au Akaunti inasoma (negative balance) ikiwa ni 'over draft facility'