Shalom wana wa Mungu!

Naamini MUNGU ameendelea kuwa mwema kwenu akiwatetea katika yote kama ilivyo kawaida yake kwetu tumtumainiao.

Wale waliokuwepo mwaka jana December wakati tunasherekea miaka 50 ya uhuru kwenye maombi ya kuombea taifa, London Vision House watakumbuka jambo hili. Tulitangaza kuwa tutaendelea kila mwaka wakati wa kusherehekea uhuru tutakuwa na siku ya kuombea taifa. Wale waliohudhuria mwaka jana mnakumbuka kuwa tulikua na wakati mzuri sana wa maombi na kushikiana maneno ya Mungu pia.

Umefika tena wakati ule wa kusherehekea miaka ya uhuru, hebu tujumuike pamoja tena kuombea taifa. Nawatia moyo ndugu zangu, tuache kukaa pembeni na kulalamika, tufanye sehemu yetu kwa mamlaka tuliyopewa katika Neno la Mungu. Utakumbuka habari ya Lutu na Sodoma na Gomora, unajuaje maombi yako yatakuponya wewe na familia yako hata kama wengine wakikataa kutubu? Mungu anajibu maombi, hebu na tukutane kumuomba Mungu aiponye nchi yetu katika maovu na manyonge yote yanayotukera kila siku!


Maombi haya ni ya watu wote wa madhehebu yote wanaoamini maombi yanabadilisha hatima ya taifa! tafadhali kusudia kushiriki na watanzania wenzako katika siku hii ya muhimu ya kubadilisha mwelekea na hatima ya watanzania wote.

Maombi ya mwenye haki yafaa sana akiomba kwa bidii...YAKOBO 5:16

Ubarikiwe ukusudiapo kuhudhuria na kushiriki maombi haya.

Sis. Flora For CITE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...