Watanzania wanaoishi jijini New York na Vitongoji vyake wakiwamo wawakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, jana Jumamosi, waliungana na Familia ya Bw. Emmanuel Alfred Swere na Bi. Doto na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, katika Ibada ya kumuaga Jesca Emmanuel (12) aliyefariki ghafla Jumapili iliyopita.

 Ibada ya kumuaga Jesca ilifanyika Bergen Funeral Home na iliongozwa na Mchungaji Perucy Butiku. Mazishi ya Marehemu Jesca yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne katika kijiji cha Bumbombi- Tarime Tanzania. Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie Apumzike kwa Amani. Amina
Mama mzazi wa Jesca  Bi. Doto akilia kwa uchungu mara baada ya kuona  mwili wa mtoto wake.
Baba  mzazi wa  Jesca, Bw. Emmanuel akilia kwa  uchungu mara baada ya kumwona mtoto wake, pembeni yake ni Shangazi wa Jesca, Bi. Rose
 Mchungaji Perucy Butiku akiongoza Ibada ya  kumuombea Marehemu Jesca Emmnauel na kuwafariji wazazi wake, ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waombolezaji kwamba kila mmoja wetu anasiku yake atakayoitwa na  Mwenye-Enzi Mungu,  kama alivyoitwa Mtoto  Jesca, ni siku ambayo hakuna mtu aijuaye. Na kwa sababu hiyo akasisitiza  umuhimu wa kujianda. Ibada ilifanyika siku ya Jumamosi Bergen Funeral Home jijini New York.
 Mdogo wake Jesca, Catherine akiwa ameelemewa na majonzi mazito kwa kuondokewa na dadayake, Catherine  aliwatia uchungu waombelezaji pale alipomuaga  Dada yake kwa  kutamka  "  Bye Jesca". 
Brigedia Jenerali Maganga Mwambata Jeshi  katika  Ubalozi wa Tanzania nchi Marekani, akiaga. Brigedia Jenerali Maganga ni kati ya   Maafisa  wanne waliowakilisha  wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
 
 Balozi   Tuvako  Manongi   akiungana na waombelezaji wengine  kumuaga marehemu Jesca. Baada ya  ratiba ya kuaga,  Balozi Manongi aliwashukuru watanzania kwa ushirikiano, upendo na mshikamano mkubwa waliouonyesha wakati wote wa kipindi cha maombolezo ya msiba huo na akawasihi kuendeleza umoja huo

 Bw. Emmanuel na Bi.  Doto wakiwa na mtoto wao,  muda mfupi kabla ya sanduku kufungwa 
Sanduku   lenye mwili wa Jesca tayari kwa Safari ya kwenda  Bumbombi- Tarime Tanzania kwa Mazishi.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Wapendwa wazazi Mungu awatie nguvu na faraja yake ijae mioyoni mwenu. Ni ngumu sana mnapomzika mtoto wenu tena kwa umri mdogo. Nasi tuliondokewa na mtoto mdogo ila faraj ya Mungu pekee ndio imetusimamisha tena. Poleni tena wazazi na familia yote
    Nodla

    ReplyDelete
  2. Poleni sana sana jamani kwani hata mie imenitoa machozi kwa kifo cha mtoto Mpendwa wenu. RIP Jesca

    ReplyDelete
  3. Tunawapo Pole wazazi wa marehemu na familia yote kwa ujumla,pia salamu za pole kwa ndugu jamaa marafiki, na watanzania wote kwa ujumla.

    Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu

    ReplyDelete
  4. Poleni sana wafiwa wote. Mungu awape faraja. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe.

    ReplyDelete
  5. Poleni sana wazazi wenzetu kwa kuondokewa na binti yenu mliyempenda Jesca.

    ;Lakini ndugu hatutaki msijue habari zao waliolala mauti msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini''

    Jesca hajafa amelala katika kristo naye tutaonana naye paradiso.

    Mungu awatie nguvu sana na kuwafa faraja wakati wote wa huzini kubwa mioyoni mwenu.

    Poleni sana.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana wazazi, ndugu na marafiki... Inatia huzuni sana kupoteza mtoto mdogo hivyo.. Mungu ailaze roho ya Jesca mahala pema peponi... Amina

    ReplyDelete

  7. Mungu awatangulie na kuwapa amani na faraja yake.

    ReplyDelete
  8. Napenda kutoa pole zangu kwa moyo mkunjufu kabisa.
    mimi siwafaham nyinyi ndugu zangu mlioko Nee York.
    lakni napenda kuwajulisha tuko wote,katika kipindi hiki kwa sala na majonzi.Mungu atawapa nguvu.
    Imeniuma sana kama,simfaham Jesca lakni ni mtoto mdogo kutangulia mbele za haki pamoja kufa hakubagui.

    Mungu awape nguvu,nawaombea na namwombea Jesca alale salama.

    ReplyDelete
  9. Poleni sana wazazi! Poleni sana! I am just wordless

    ReplyDelete
  10. Poleni sana Wazazi, Catherine, na familia yote. Mungu awape nguvu ya pekee katika kipindi hiki kigumu. Na amlaze Jesca wetu mpenzi mahali pema peponi amina.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...