Kaimu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Longinus Rutasitara (katikati) akifafanua jambo wakati wa mkutano na Wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na wadau wengine (hawapo pichani) kujadili misaada ya Serikali ya China katika kuisadia Tanzania kutekeleza miradi mikubwa katika sekta kama vile Kilimo, Miundombinu na Umeme. Wengine katika picha ni Maafisa Waandamizi kutoka Tume hiyo.


Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano na ujumbe kutoka Serikali ya China kuhusu kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi yake mikubwa. Wengine katika picha ni Bw. Lin Zhiyong (katikati) Mwakilishi Mkuu katika masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini na Bi. Fang Wang, Afisa kutoka Ofisi hiyo.

Bw. Lin Zhiyong akitoa maoni yake wakati wa majadiliano hayo.

Balozi Kairuki na wajumbe kutoka China wakimsikiliza Kaimu Katibu Mtendaji, Bw. Rutasitara (hayupo pichani) wakati wa majadiliano. Wengine katika picha ni Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Tume ya Mipango walioshiriki mkutano huo.

Bw. Rutasitara na Maafisa wengine wakimsikiliza Bw. Li wakati wa majadiliano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...