Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman aliongoza Ubalozi wa Tanzania nchini Oman katika ya chakula alichoaandaa nyumbani kwake Shatti Al Qurum, mjini Muscat Oman kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaaga wajumbe wa mkutano wa Diaspora uliofanyika mjini muscat kuanzia Alhamis tarehe 20 Disemba na kumalizika siku ya jumamosi tarehe 22 Disemba 2012 katika ukumbi wa Sindbad, Crowne Plaza Hotel Muscat.
Katika hotuba yake ya kuwakaribisha wageni wake Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh aliwapongeza wajumbe wote kutoka Tanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kukabili hoja na kero mbalimbali za wana diaspora, wafanya biashara na wawekezaji wa Oman kwa manufaa ya nchi ya Oman na Tanzania, michango yao na mahudhurio yao katika mkutano huu wa Diaspora ambao umefanyika kwa mafanikio makubwa.
Pamoja na pongezi hizo Mheshimiwa Balozi Ali Saleh aliwasisitiza wajumbe hao kuendelea kufanya juhudi katika kufuatilia na kutekeleza yale yote yaliyokubaliwa katika vikao vya mikutano iliyofanyika.
Aidha kwa upande Mheshimiwa Balozi aliwashukuru wana Diaspora kwa ushirikiano wao mkubwa na uvumilivu waliounyesha wakati wote wa mikutano hiyo.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu ulijumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na taasisi kadhaa kutoka sekta ya umma na binafsi ikiwa ni pamoja Shirika la utangazaji Tanzania, Bodi ya Utalii, Benki yza CRDB, Azania Bank Corp, Bank of Africa, Benki ya Watu wa Zanzibar, Zanzibar Insurance, Zanzibar Social Security Fund, Zanzibar Chamber of Commerce, Tanzania Investment Centre, Zanzibar Investment Promotion Authority na Tanzania Private Sector Foundation, Dar Es Salaam Maritime Institute.
Mheshimiwa Balozi Ali Saleh ( wa
pili kutoka kushoto) akifunga kikao cha mwisho cha mkutano wa Diaspora nchini
Oman . wa kwanza kushoto ni Mhe. Balozi, Bertha Somi, Mkurugenzi wa Idara ya
Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje
Wajumbe wa mkutano
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi
wa Tanzania nchini Oman ( aliesimamama ) akizungumza na ujumbe wa Tanzania na
wana diaspora katika hafla ya chakula cha usiku
Juu na chini ni Wajumbe wa mkutano wa Diaspora ya Oman wakimsikiliza Mheshimiwa Balozi
wakati wa Sherehe ya kufunga mkutano
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...