Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akifafanua jambo wakati wa mkutano wake wa mwisho wa mwaka na Klabu ya Waadishi wa Habari wa Umoja wa Mataifa ( hawapo pichani). Katika Mkutano huo ambao ulifanyika siku ya jumatano aliutumia kuelezea mafanikio na changamo za utendaji kazi wa UM katika mwaka unaomalizika. Pia alielezea jitihada anazozifanya katika kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa eneo la Mashiriki ya DRC. Akabainisha kwamba katika siku tano zilizopita amekuwa akifanya mazungumzo kwa njia ya simu na baadhi ya viongozi wa Afrika kwa lengo la kupata mchango na maoni yao kuhusu mpango mpana wa kisiasa anaojaribu kuuanda kwajili ya DRC hususani eneo la Mashiriki. Miongoni mwa Marais ambao Ban Ki Moon amefanya nao mazungumzo ni Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Home
Unlabelled
Ban Ki Moon ataka mtizamo mpana katika kuisaidia DRC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Jamani jamani Ban awe na aibu kidogo. Hivi jeshi la UN linafanya kazi gani huko Mashariki ya DRC? jeshi linakuwa wapi mpaka waasi wanauteka mji wa Goma, pili ule wa Sake kiurahisi namna ile? halafu nasikia bajeti ya hili jeshi ni kubwa mno. Wananchi wa DRC hawaoni manufaa ya jeshi hili. Wanaonufaika ni walioko makao makuu ya UN New York, ambao wanashughulika na "paper work" za kitengo hiki cha Monusco. Imprest kwa wingi. Mungu Ibariki DRC
ReplyDeleteNi aibu kubwa kuona JESHI la Umoja Wa Mataifa limekaa mashariki mwa Kongo zaidi ya miaka 20 mpaka leo limeshindwa kuweka AMANI...Hao FDLR(Jeshi la Ukombozi la Rwanda),CNDP na M23(jeshi la Rwanda) kati yao ni Wakimbizi kutoka Rwanda wengine walipewa hifadhi ya Ukimbizi kwa convention ya Geneva(UN)nchini Kongo,wameigeukia nchi ambayo imewapa hifadhi... cha kushangaza Uasi wao kuliko waufanyie nchini mwao...Wananchi wa Kongo ndo wanauwawa kikatili !!!!
ReplyDeleteNdugu Ban Ki Moon,UN itakachokifanya ni kuwarudisha hao FDLR ma kwao Rwanda.Hao CNDP,M23 na FDLR wafunguliwe mshtaka katika mahakama ya UN Hague ao Arusha kwa mauwaji ya kinyama wanayoifanya Kongo toka Agosti 1998 mpaka leo!!!