TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII ASUBUHI HII  TOKA PANDE ZA  KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM  ZINAELEZA KUWA WATU WAWILI WAMEPOTEZA MAISHA NA MMOJA KUJERUHIWA MGUUNI BAADA YA MAJAMBAZI KUVAMIA GARI MOJA DOGO LILILOKUWA LIMEBEBA HELA NA KUZIPORA.

MAJAMBAZI HAO WALIMPIGA RISASI NA KUMUUA  MMILIKI WA GARI HILO PAPO HAPO BAADA YA KUTOKEA MALUMBANO, WAKATI WALIPOKUWA WAKITAKA KUFUNGULIWA GARI HILO HUKU YEYE AKIKATAA.

NA WALIPOFANIKIWA KUCHUKUA HELA HIZO WAKAPIGA MBIO HUKU WANANCHI WENYE HASIRA WAKIWAKIMBIZA. KUONA HALI INAKUWA MBAYA UPANDE WAO, MAJAMBAZI HAO WALIANZA KUPIGA RISASI HOVYO  AMBAPO MOJA ILIMKUTA MTU MMOJA KICHWANI AMBAYE ALIPOTEZA MAISHA PAPO HAPO NA MWINGINE AKAPIGWA NA KUJERUHIWA MGUU.

JESHI LA POLISI LILIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUANZA KUFUKUZANA NA MAJAMBAZI HAO AMBAO WALIFIKA SEHEMU NA KUZITELEKEZA HELA HIZO NA KUINGIA MITINI.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA TUKIO HILO NA TUTAKUWA TUKIPEANA TAAFRIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hela ni muhumi zipatikane ili ziwe ndio Ushahidi wa wizi!

    Isiwe waqpatikane Majambazi halafu hela zisionekane, hiyo hapana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...