Habari za leo kaka michuzi,natumai hujambo na unaendelea vizuri na majukumu yako ya kujenga taifa letu.
Kaka naomba niwasilishe hii hoja kama kero yangu kwa mwaka huu, mimi kama mkazi mwenyeji wa Kilimanjaro nasikitika mno mno jinsi mkoa wetu unavyolea wahalifu bila aibu na kuwapa ujeuri wa kuona mwenye pesa haguswi.
Mifano ninayo mingi sana lakini mfano hai mmojawapo ni hawa vijana wanaosafirisha waethiopia na wasomali,inasikitisha sana sana wanaohukumiwa ni wale ‘’nyoka’’ wao ambao wanatumwa kuendesha magari lakini wale ‘’mapapa’’ wa hiyo biashara wanaachwa wazi kabisa na wala sheria haiwakuti. Hivi jamani mti wenye sumu utaukata matawi ufe bila kufikia mizizi? Wahabeshi waliokamatwa mwaka jana desemba Morogoro, walioishia kuhukumiwa ni dereva na utingo,je mwenye gari ambaye ni muhusika mkuu na mkazi wa kilimanjaro aliitwa hata kuhojiwa? uhamiaji haina taarifa za hii habari? Unaweza kuona fika michezo michafu inavyoendelea. Muhusika wala hatishiki na Bado tunamuona anavyotapanya hela haramu,huku ‘’nyoka’’ wake wakisota kutumikia kifungo gerezani.mifano mingine ni mingi ila kwa huu unatosha,
Huo ni mfano mmoja mdogo. Ushauri wangu kwa jeshi la polisi na taasisi nyingine za kisheria tunaomba hii tabia ya kuchekea wahalifu ikomeshwe. Tusisubiri hadi maafa yatokee ndo tuanze kunyoosheana vidole. Mkoa wa kilimanjaro tubadilike,tusikubali kulelea wahalifu!
Naipenda Tanzania,naipenda michuzi blog.
Merry christmass
mdau
Mdau wa Kilimanjaro ahsante sana!
ReplyDeleteHII NI SALAMU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA TOSHA KWETU!
YAANI KWA UZITO WA MAKALA HII HATA BALOZI WA JAMVI HILI MHE. ANKALI MICHUZI AMEWEWESEKA NA AKAPOSTI MARA 9 HIVI!
-----------------------------------
HAKUNA JINSI NI WAKATI SASA WA KUYASHUGHULIKIA MAAZIMIO YOTE KUHUSU WAHALIFU KIUJUMLA BAADA YA AHADI NYINGI NA SASA MUDA UMEPITA SANA.
TUNGEFARIJIKA SANA KWA KUANZA ANGALAU HIYO NGAZI YA WAHUSIKA WAKUU 'MAPAPA' WASAFIRISHAJI HARAMU WAKAFIKISHWA KWENYE SHERIA ILI IWE SALAMU YA KRISMASI KWETU NA MWAKA MPYA 2013 !!!
ANGALUA NA SISI WANANCHI TUFARIJIKE!
ukiishia kusema mapapa haisaidii kama una taarifa ni vizuri kuwataja. maana wengi wanalalamika hata wanasiasa wenyewe lakini ni lazima tubadilike tutoe ushahidi wa kutosha kuwahukumu la sivyo tutaishia kuwashangilia tu
ReplyDeleteNi wakati sasa kuhakikisha Mabasi mapya ya Idara ya Magereza, yanatumika kwa TIJA badala ya kuchoma mafuta na kuingizia Serikali gharama yawe yanawabeba wakusudiwa (Mafisadi Papa) badala ya wezi wa simu za mikononi, wezi wa mifukoni na wezi wa kuku vichochoroni.
ReplyDelete-----------
TUTAFARIJIKA SANA KUONA TUNASHIRIKIANA KUWATAJA WAHUSIKA, MAMLAKA ZINAPATA UJASIRI ZINAJITOA MUHANGA WANAKAMATWA NA HATIMAYE WANAJIKIUTA WANAJAZANA KWENYE MABASI YA MAHABUSU WANACHUKULIWA HATUA NA WANAFUNGWA.
-----------
KWA NINI ISIWEZEKANE?
KAFUNGWA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ITALIA BILIONEA SILVIO BERLUSCONI ITAKUWA MAFISADI WETU HAWA WA KITOTO WA GENGE LA KARATA TATU?
NI WAKATI WA KUWATUMIA WAHALIFU WA ISHU ZA KITOTO KWA VIFUNGO VYA NJE VYA MANISPAA ILI WASAFISHE MAZINGIRA NA KUZIBUA MITARO KWENYE MAKAZI YETU, HUKU NAFASI ZA SITI ZA VITI VYA KWENYE MABASI WAKIKAA WAHUSIKA KAMILI (MAFISADI)!
------------
Kutoka Usafiri wa Makarandinga miaka ile hadi Mabasi ya Kisasa ya Mahabusu ni hatua ndogo?
Ni MAENDELEO MAKUBWA NCHINI TANZANIA BONGO TAMBARALE!!!
Angalau mmoja kati ya walalamikiwa wakubwa wa Ufisadi kuanzia ngazi ya chini kama hawa Mwakala wa Usafiri Haramu hadi ngazi ya Taifa angechukuliwa hatua tungalifarijika saaana!
ReplyDeleteLakini wapi!
Nchi zilizoendela ili kufika pale walijitoa Muhanga kishujaa:
ReplyDeleteITALIA:
Waliwaua Mafashisti ambao walikuwa wanapinga maendeleo na kukwamisha jitihada na kuimarisha Ubeberu.
UFARANSA:
Waliwaua Mabeberu wachache waliokuwa wamemiliki karibu ardhi yoote ya wananchi, huku wengi wakibaki hohe hahe.
UINGEREZA:
Waliwaua Makabaila walihodhi ardhi yote na kuwaacha Mabepari wenye Viwanda ambao walikuwa na faida kwa mali wanazozalisha na nia yao njema kuleta maendeleo.
Hivyo ni zamu sasa ya TANZANIA kujitutumua ili itoke kwenye vikwaqzo vya zama zetu UFISADI, (SISI HATUTAWAUA, TUTAWAKAMATA TUTAWAFILISI MALI ZILIZO ZA WIZI NA KUWAFUNGA) na sisi tunalazimika kujitoa muhanga ili tusonge mbele!
Kama una uhakika na una ushahidi kwamba huyo mwenye gari ndiye muhusika mkuu, wakilisha ushahidi wako kwenye vyombo husika. Hayo ndiyo mapambano, na kila mtu ana wajibu wake. Kuna mdau mwenye hasira kali dhidi ya usfisadi kule TBS alionyesha uzalendo mkubwa kwa kuanika maovu ya TBS, na hatua zilichukuliwa kwa kiwango chake, au sio? Kulalama pekee haitoshi.
ReplyDelete