Baadhi ya Majeruhi waliojeruhiwa na Majambazi mapema leo katika eneo la Kariakoo,jijini Dar wakiwa kwenye gari la Polisi tayari kwa kupelekwa hospitali kwa Matibabu.kwa mujibu wa Ripota wetu ni kuwa Baadhi ya Majambazi hao wamekamatwa na wapo kwenye kituo cha Polisi Msimbazi Kariakoo.Majambazi hao wameuwa watu wawili kwa risasi. 
Wananchi wa jiji la Dar wakiwa wameduwaa bila kuamini kile walichokiona kikitokea mapema leo eneo la Kariakoo,baada ya Majambazi kuvamia gari moja lililosadikiwa kuwa na hela walizotaka kuziiba na kupelekea kuuwa watu wawili papo hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. POLISI YA SASA NI DOT.COM

    POLISI INATISHA!

    POLISI YA SASA SIO ILE YA MAFAILI YA KARATASI NA MAKABRASHA, INATUMIA KOMPUTA!

    POLISI NGUNGURI!

    POLISI SIO MCHEZO!

    Majambazi nawashauri mtafute akili mpya mkaombe Makazi mapya Vijijini mkalime, biashara ya Ujambazi itawaponza mutakufwaaaaa!!!

    ReplyDelete
  2. Mungu awaweke mahala pema peponi walio poteza uhai wao. Na naamini haki itatendeka. Hongera polisi ya bongo Mungu awape nguvu ya kuweza kulinda usalama wa raia wa tz kikwete ooooyeeee.

    ReplyDelete
  3. Sasa mdau unaisifia polisi na huku watu washapoteza maisha? ilipaswa wazuie tukio au ndo unatumia fasihi...

    ReplyDelete
  4. Kwanza huyo mdau ana uhakika na anachokisema? kwa lipi hasa? aaaahh nadhani yupo usingizini anaota ndoto za mchana kweupeeeee.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Pili (2) Tue Dec 18, 09:58:00 PM 2012 na Mdau wa Nne (4) Wed Dec 19, 02:22:00 AM 2012

    ...UJAMBAZI SASA MNATAKA APAMBANE NAO NANI?

    SAWA, PAMEKUFA WENGINE WASIO NA HATIA JE, MKITAKA MAJAMBAZI WASISHUGHULIKIWE WENZETU MPO UPANDE GANI?

    1.MPO KATIKA HAKI ZA KIBINAADAMU?

    AU

    2.MPO KATIKA MSIMAMO WA KIDINI?

    JE, HAKI ZA UBINAADAMU NA MISIMAMO YA KIDINI VINAKUBALIANA NA MASUALA MABAYA YA NYETI KAMA UHALIFU NA UJAMBAZI ???

    ReplyDelete
  6. Majambazi yaliiba pesa?kama yaliiba unafikiri mwenye pesa atarudishiwa zote?nyingine zitadondokea njiani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...