Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (katikati) akizungumza na wafanyakazi na familia zao katika sherehe za Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi. Wengine
ni viongozi wa ngazi za juu wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru akiwania mpira pamoja na mfanyakazi wa benki hiyo, katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
 Watoto wa wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakishindana kufukuza kuku ili kumpata mshindi katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
 Wafanyakazi na familia zao wakiselebuka katika sherehe za Siku ya Wanafamilia wa NBC jijini Dar es Salaam juzi.
Hapa watoto wakionyeshana nani ni mkali katika kusakata muziki kwa kutumia mtindo maarufu ujulikanao kwa jina la ‘Kiduku’ uliofanya sherehe hizo kunoga zaidi.
 Wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakishindana kuvuta kamba ili kumpata mshindi katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo ijini Dar es Salaam juzi.
‘Father Christmas’ akigawa zawadi kwa watoto wa wafanyakazi wa benki ya NBC Katika sherehe ya Siku ya wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Big up NBC. I like it. 2gether as one.

    ReplyDelete
  2. Ohooo,

    Mkurugenzi wa NBC, Ndugu L.Mafuru unafiti kote kote!

    Mkurugenzi wa Benki kweli Mpira unauweza!!!

    Tumepoteza Kombe la CECAFA buree Uganda wiki iliyopita kwa nini wasingekuweka Kikosini Kili Stars?

    ReplyDelete
  3. hapo ndio huwa nafurahishwa na sisi wabongo, michezo ni kuvuta kamba na kukimbiza kuku na ulimbwende!!

    ReplyDelete
  4. Masuchaaa,
    Nia mwanangu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...