Kanisa la St Annes Lutheran katikati ya jiji la London juzi Jumamosi lilikuwa kituo maalum cha kumwaga na kuwa wasifu wa maisha ya marehemu Freddy Alex Mtoi (pichnai) aliyekuwa mtangazaji wa BBC Swahili kwa miaka mingi.
Ibada hiyo iliyoendeshwa na wachungaji Tumaini Kalaghe na Mathew Jutta, ilihudhuriwa na wanahabari mbalimbali kutoka BBC , Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania, Clement Kiondo, marafiki wa karibu waliomjua marehemu na wanananchi wa sehemu toka Tanzania, Afrika na Ulaya.
Mratibu wa mazishi , Zawadi Machibya, ambaye ni mtangazaji wa BBC, mzawa wa Tanzania , aliendesha shughuli na kuwajulisha wasemaji wote waliozungumzia kwa kuanza kueleza namna neno “mtanashati” lilivyomvaa Freddy Mtoi aliyefariki usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 17 Novemba, 2012.
Mchungaji Mathew Jutta alikumbusha kwamba safari yetu wanadamu huanzia kwa Mungu na kuishia kwa Mungu. Akailinganisha nsafari hiyo na ile ya kutoka nyumbani Afrika kuja Majuu (ambapo paliitwa Mtoni enzi mchungaji alipokuja Ulaya takribani miaka 20 iliyopita). “Kwa wanaobakia ni huzuni lakini kwa anayesafiri ni furaha yenye matumaini.” Akimzungumzia marehemu alitaka zaidi kututuliza roho tuliyobakia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...