---
Kundi la Jahazi Modern Taarab chini ya kiongozi wake, Mzee Yusuf ' Mfalme' usiku wa 'Boxing Day' lilifanya makamuzi ya nguvu ndani ya ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kuzikonga nyoyo za wapenzi wa taarab waliofurika mahali hapo. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyochukia nafasi wakati wa shoo hiyo.
(PICHA: ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)
Jana nilifunga safari kwenda kushangaa hii Dar live.Show hii ilikuwa nzuri,ukumbi mzuri,huduma nzuri.Mahudhurio 60% akina Dada na 40% akina Kaka.Kinachoendelea humo ukumbini siyo taarabu tu(Tafakari).Ni balaa.
ReplyDeleteDavid V
Mdau hapo juu kwa kuangalia picha hapo juu mimi naona wanaume ni 80% na wasiochana ni 20%. Haya ni mapinduzi ya kuhuzunisha katika Taarabu.
ReplyDeleteHEEE DAVID V, umerudi eeh kwa umekuja holiday eeh? nitakusakane eb michu muweke huyu mdau humu tumuone ukute tushapishana naye maeneo bilakujua, nahamu yakumjua kaswaaaaaa kama baraka wa chibiriti.
ReplyDeleteYeah nimekuja holiday Dar(Kwetu kuzuri),napata tabu sana na joto la Daresalaam.Na siyo joto kusema kweli-Ni humidity(Unyevu?).Unyevunyevu upo juu sana Daresalaam kipindi hiki.Tutakutana tu bado nipo hadi katikati ya January 2013.Nawatakieni wote heri ya mwaka mpya 2013
ReplyDeleteHilo kundi linalocheza hapo ni asilimia 10 tu ya watu wote waliokuwemo ukumbini.
David V