Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava akifungua mafunzo kwa watendaji kutoka taasisi za utafiti wa vyakula na magonjwa ya binadamu kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kutokana na bioteknolojia ya kisasa. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya Giraffe Ocean View, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa warsha ya Tathmini ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na teknolojia za kisasa wakifuatilia mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais - Idara ya mazingira. Mafunzo hayo yanaendelea katika Hotel ya Giraffe Ocean View, jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mafunzo ya Tathmini ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na bioteknolojia za kisasa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (wa tatu kutoka kulia) mara baada ya kufungua mafunzo hayo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (kulia) akibadilishana mawazo na Dk. Flora Ismail kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dk. Julius Ningu, Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kufungua mafunzo kwa watendaji kutoka taasisi za utafiti wa vyakula na magonjwa ya binadamu kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kutokana na bioteknolojia ya uhandisi jeni. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya Giraffe Ocean View, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...