Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiakata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto
katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012.
Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto
katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmoja wa walionufaika na hatua ya serikali ya kujenga nyumba mpya 35 kwa ajili ya waathirika wa mabomu Gongo la Mboto
katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012. Mama huyu ambaye alipoteza mume, amejengewa nyumba ya vyumba vitano pamoja na fremu ya duka.
Baadhi ya nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto
katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala kama zinavyoonekana leo Desemba 13, 2012 baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
PICHA NA IKULU
kila siku lawama na matusi kwa serikali leo iko haja ya kutoa pongezi kwa moyo mkujufu kwa serikali na rais kwa uamuzi huu wa kiungwana na haki kwa waathirika serikali yetu haina budi kuwa ya kiungwana sana na kuwatendea haki wananchi pale inapostahiki hasa ikiwa kosa lipo upande wa serikali au hapana kwani raia wanapoathirika na taifa linaathirika.
ReplyDeletemdau.kwa obama.{hawaii}
Good job....Job well done JK
ReplyDeleteHAYO NDO MAMBO MH RAIS NA SERIKALI YAKO..TUNACHOHITAJI:
ReplyDelete1. NI KASI ZAIDI YA KUHAKIKISHA KUWA KILA MWANANCHI ANAKUWA NA BIMA ILI AKIPATA TATIZO FIDIA IWEZE KUMSAIDIA KUJIKWAMUA KATIKA MATATIZO YALIYOMKABILI
2.KUHAKIKISHA KUWA UTOFAUTI KATI YA WALICHO NACHO NA WASIOKUWA NACHO UNAPUNGUA KWA KUHAKIKISHA KUWA RASILIMALI ZETU ZINATUMIKA VIZURI KUJENGA NCHI NA KUWAPATIA WATANZANIA AJIRI
Naafiki maneno mazuri ya mdau. Serikali hii imefanya mambo mengi mazuri ambayo hatuna budi kuipongeza pamoja na mapungufu machache ambayo wengi tumekuwa tunayoona na kutupia lawama kwa haraka. Mungu ibariki Tanzania kwani tutafika tunakotaka japo hata kwakuchelewa ila kwa makini, amani na utulivu.
ReplyDeleteWapinzani na hili hawaoni, waone aibu basi wasifie hata kidogo... walikuwa wa mbele kukashifu sasa kuna nyumba kimyaaaa! Kada wa CCM
ReplyDeleteTujifunze kushukuru!
ReplyDeleteSio siri hatua hii ni kubwa mno kufanywa nchini, lazima tukiri ya kuwa jambo jema na la busara limefanywa chini ya Utawala wa Serikali ya JK!
Hongera JK NA SERIKALI KWA UJUMLA!
mimi ni mfuasi wa chadema na mpenda maendeleo,kwa anachofanya huyu rais wetu nashangaa kuona watu wakilaumu na kumbeza mpaka kunifanya kushindwa kuelewa ni kwanini analaumiwa sana na watu, kana kwamba atendi jambo lolote la maendeleo na manufaa katika nchi hii.Kiukweli mambo aliyoyafanya katika uongozi wake ni makubwa mno,kitendo kama cha hapo juu ni mara chache kuona serikali ata za nchi zinazotuzunguka zikikifanya,Big up JK,tutakukumbuka sana mzee wetu.
ReplyDeleteKIMYAAAAAA
ReplyDeleteHAYA SASA,
WANAFIKI UTAWAONA KTK MAMBO KAMA HAPA SASA.
WAO WAMEKAA KAZI KUTMU MAONI YA LAWAMA NA KEJELI, MBONA NYUMBA ZINAKABIDHIWA MMEKAA KIMYA?
LAZIMA MUWE WANA SIASA WENYE MWAMKO KAMA MWENZENU WA CHADEMA MWENYE BUSARA HAPO JUU WA 7 SILVESTER ALEX !
MSIWE MBELE KWENYE LAWAMA NA DHARAU, KUWENI WAKWELI NA WAAMINIFU HATA KWA KAULI !!!
Ingekuwa pana uwezekano wa kuipindisha Katiba Kipengele cha Uraisi ningeomba Mhe. Raisi JK aongoze kwa miaka kama 15 au 20 hivi kwa uchache!
ReplyDeleteSio siri tutamkumbuka sana Kikwete kwa mengi!