Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short (kushoto kwa Rais), Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband (kulia kwake), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan wakiangalia bada ya mkutano wa na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short, Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband, Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. HAHAHA... HATA JUMA KASEJA( AU YEYOTE ) JIHIMU NENDA UINGEREZA UKUTANE NA WAZIRI MKUU UMPELEKEE JEZI.

    ReplyDelete
  2. JEZI NYINGINE. U gotta love our president.

    ReplyDelete
  3. SUNDERLAND ya Uingereza kwa Tanzania ndio MSIMBAZI YENYEWE!

    Hivyo kuipokea jezi yao ndio KAMA UMESAINI na ndipo Mwana Yanga Imara unajikuta bila kuelewa unaelekea Klabu ya SIMBA S.C tena hata ukitakaa kwa pesa utaenda kwa Mkopo!

    ReplyDelete
  4. Manji anauliza, JK janja hii kwisa jua?

    Simba SC inakuja kwa mlango wa Jikoni hapo!

    ReplyDelete
  5. Ha,ha,ha,ha !

    Niliwahi kushuhudia tukio moja la kusisimua kwa Fundi Viatu.

    Palikuwa na ndara (kandambili)jozi kadhaa katika gunia za Wateja kuvaa kwa muda kwa fundi viatu wanapopigiwa kiwi viatu vyao.

    1.ALIFIKA MTEJA WA KWANZA:
    FUNDI VIATU AKAFUNGUA GUNIA LA NDARA AKATOA NDARA ZA KIJANI, AKAZIRUSHA MIGUUNI MWA MTEJA WA KWANZA YULE MTEJA ALIPOONA NDARA ZA KIJANI HEWANI, ALIZITAZAMA KWA TAHADHARI AKAZIKWEPA ZIKATUA CHINI, AKAZIRUSHA KURUDI KWA FUNDI AKADAI NIBADILISHIE!, MZEE MMOJA ALIKUWEPO AKAMWAMBIA FUNDI BADILI RANGI FUNDI AKATOA NDARA NYEKUNDU ALIPORUSHA MTEJA AKAZIDAKA KWA FURAHA KABISA.

    2.AKAJA MTEJA WA PILI:
    AKAMKUTA MTEJA WA KWANZA ANA NDARA NYEKUNDU MIGUUNI AKAZITAZAMA SANA HUKU HAJAFURAHI USONI, MTEJA WA PILI
    AKARUSHIWA NDARA NYEKUNDU, WAKATI ZIPO HEWANI AKARUSHA TEKE KUZIRUDISHA KWA FUNDI, ZIKATUA KWA FUNDI, FUNDI KWA BUSARA AKARUDISHA NDARA ZA KIJANI KWA KUZIRUSHA,,,MTEJA AKAZIPOKEA KWA KUZIDAKA KAMA KIPA WA TIMU YA MPIRA ANAVYODAKA!

    HIVYO TUKAJUA YA KUWA UNAZI WA TIMU ZA MICHEZO UPO HADI KTK MAISHA YA KAWAIDA!

    JE, MHE. RAISI JK KTK PICHA PILI UNAONEKANA RANGI ZA JEZI(NYEKUNDU +NYEUPE) HAZIJAKUVUTIA KWA JINSI UNAVYOIKAGUA JEZI HIYO, JE JEZI HIYO ITAKAA MGONGONI MWAKO ???

    ReplyDelete
  6. Duhhh,!

    Rage na Msimbazi wana Mipango hawa si mchezo!

    Yaani wamewaita Tawi lao la Uingereza wakawatuma, wao ahhh hata hawakuwasindikiza!

    ReplyDelete
  7. Picha ya 2,

    Mhe. Raisi JK jezi kama unavyoona ndiyo hii imechapishwa jina la Cheo chako yaani 'MR. PRESIDENT' ,

    ...(SWALI) Je, ni nini cha ziada ungependa kiwepo ktk jezi, inaonyesha hujaridhika?

    ...(JIBU) ahhh ningependa iwe ktk rangi ya KIJANI NA NJANO!

    ReplyDelete
  8. KIKWETE wewe si mpenzi wa Newcastle United?sasa unashika vipijezi ya sunderland?AU hujui uadui wa hizi timu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...