Baadhi ya waombolezaji wakielekea makaburini wakati wa mazishi ya mbunge wa zamani wa Tabora mjini, marehemu Siraju Juma Kaboyonga katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Siraju Juma Kaboyonga aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,ambaye alifariki ghafla jana.
Rais mstaafu wa awamu ya nne,Mh. Mzee Ali Hassani Mwinyi akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Siraju Juma Kaboyonga wakati wa mazishi yake,yaliyofanyika mapema leo kwenye makaburi ya Kisutu,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kweli,kila Binadamu ataonja Umauti!Mareh.Siraju Juma Kaboyonga "was a very gentle damn good man!".Alikuwa mkarimu sana,msikivu,binadamu wa kweli,mpebda watu,msomi na mwana taaluma,mcheshi,mchapakazi,msemakweli,............,na mcha Mungu!Sina neno litakalo tosheleza sifa zake!Tumshukuru Mungu kwa yote,kwani,ifikapo siku ya Uamuzi wake,hakuna wa kukosoa,bali kuyakubali mapenzi ya Muumba!Rambirambi za dhati ziwafikie wana Familia,watoto aliowaacha pamoja na mama zao,ndugu na marafiki wa karibu,na wale wote aliosoma nao Chuo Kikuu cha Dar es salaam,na katika vyuo vingine,wote aliofanya nao kazi pamoja katika taasisi mbalimbali,na hakika kwa Rais Kikwete mwenyewe kwa kulipoteza "jembe hili muhimu" katika nyakati hizi za kukabiliana na Ujinga na Umaskini!Ni pigo kubwa,lakini,hatuna la kufanya.Mwenyezi Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu ndugu yetu,kaka yetu,mpendwa wetu,Mahala Pema Peponi,amina!Mungu Alitoa na sasa Ametwaa,jina lake lihimidiwe!R.I.P. Siraju!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...