Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred, ambaye yupo mjini Bukoba akikabidhi sehemu ya misaada kwa Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Msingi,Mugeza Mseto wakati alipotembelea Shule hiyo ambayo ni maalum kwa watoto wenye ulemavu ya Mugeza Mseto, inayofundisha wanafunzi wenye ulemavu.Miss Tanzania huyo pia alitembelea Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto yatima kilichopo eneo la Kashai.

Mrembo Brigitte Alfred, ambaye pia ni Balozi wa Walemavu wa ngozi, (Albinos) ametoa misaada ya kijamii katika vituo hivyo. Vifaa hivyo ni pamoja na Fimbo maalum za kutembelea walemavu wasioona, Miwani, Kofia na Madawa ya ngozi kwa ajili ya Walemavu wa ngozi. Pamoja na vyakula.

Kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam,Redd's Miss Tanzania 2012 ataelekea Mwanza kwa shughuli zingine za kijamii.
Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred (katikati) akikabidhi mafuta maalu ya kupaka watu wenye ulemavu wa Ngozi,kwa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo.Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.
Mmoja wa Watoto waosoma katika shule ya Mugeza Mseto iliopo mjini Bukoba ambaye ni Mlemavu wa Macho akipokea fimbo maalum ya kutembelea.
Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi anaeleleka katika kituo cha Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto yatima kilichopo eneo la Kashai,mjini Bukoba.Kulia ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.
Redd's Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma kwenye shule ya Mugeza Mseto iliopo mjini Bukoba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. tunawaomba REDD'S mfike vijijini ndani huko ambapo wengi hawafiki mkatoe msaada huko ambapo kuna wahitaji wakubwa zaidi ya haya maeneo ya mjini

    ReplyDelete
  2. wasiwanyanganye hizo fimbo wakawapa wazee wasio ona.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...