Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bibi. Irene Isaka (katikati) akiimba wimbo wa Mshikamano Daima pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Teophil Makunga, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania Bw. Ernest Sungura. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi cha SSRA Bw. Emmanuel Urembo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji Bibi. Sarah Kibonde Msika. Hii ilikuwa katika semina ya SSRA kwa Wahariri Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini,iliyofanyika katika Hoteli ya Tanga Beach Resort,jijini Tanga hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bibi. Irene Isaka (kulia) akijibu hoja za Wahariri Wakuu kuhusu sekta ya Hifadhi ya Jamii na Changamoto zake pamoja na Mafanikio waliyofikia mpaka sasa.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi cha SSRA Bw. Emmanuel Urembo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji Bibi. Sarah Kibonde Msika.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Teophil Makunga akielezea jambo kwa Wahariri Wakuu wa Vyombo vya Habari kuhusu umuhimu wa elimu kwa Umma juu ya sekta ya Hifadhi ya Jamii katika semina ya SSRA hivi kaibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji,Bibi. Sarah Kibonde Msika akiwasilisha Mada kuhusu Muundo wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa Wahariri Wakuu wa Vyombo vya Habari jijini Tanga hivi karibuni.
Bw. Salim Salim kutoka Jukwaa la Wahariri akichangia katika Mada ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Bw. Balinagwe Mwambungu kutoka gazeti la RAI akichangia mada katika semina ya SSRA kwa wahariri wakuu.
Baadhi ya Wahariri Wakuu wakifuatilia kwa makini mada zilizowasilishwa na SSRA katika Semina iliyofanyika jijini Tanga hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...