Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Walioathirika kwa Ukimwi cha Tocha +, Saad Ramadhan (kulia) na Arnold Goha wakiwasha mshumaa na Mratibu Mkuu wa Kifua Kikuu na Ukimwi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Hakimu Mwaikasu, wakati wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL, Keneth Wanyoto. Zaidi ya watu 400 walipima Virusi vya Ukimwi siku hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam.![]() Banda lililowekwa na TBL katika Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam ili wafanyabiashara washiriki kupimwa virusi vya Ukimwi. Mkazi wa Ilala Mchikichini, Abdalah Lukali (58), kushoto, akichukuliwa damu na Mshauri Nasaha kutoka Amref, tayari kupimwa virusi vya Ukimwi katika banda lililowekwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...