Mfanyakazi wa duka la Vodacom lilipo barabara ya Samora, Bi.Mwanahawa Juma (kulia)akimpatia maelekezo mmoja wa wateja aliefika katika duka hilo mara baada ya kuzinduliwa rasmi hapo jana.
Baadhi ya wafanyaka wa duka jipya la Vodacom lilipo barabara ya Samora, wakitoa huduma mbalimbali kwa wateja wao mara baada ya kuzinduliwa rasmi,hapo jana.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Bw.Hassan Saleh,akimkabidhi moja ya zawadi mteja ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa duka la Vodacom lililopo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam,hapo jana.
Hili ndilo duka jipya la Vodacom Tanzania lililozinduliwa rasmi jana lipo barabara ya Samora jijini Dar e Salaam.

Vodacom Tanzania imeongeza duka lake lingine na kufikisha idadi ya maduka sita katika jiji la Dar es Salaam, ambapo duka hilo linatarajiwa kukidhi ongezeko la mahitaji ya huduma kwa wateja.

Duka hilo jipya lililoko barabara ya Samora, eneo la Posta, Dar es Salaam, linatarajia kupunguza msongano wa wateja katika maduka yaliyopo sasa, likiwemo duka la Mlimani City, Mtaa wa Ohio, RDK Victoria na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Baadhi ya huduma zitakazotolewa katika duka hilo ni pamoja na kuunganishwa na huduma za Intaneti, mauzo ya muda wa maongezi, mauzo ya bidhaa na kuunganishwa na huduma mbalimbali, pamoja na kusajili kadi za simu, huduma ya M pesa na nyinginezo.

Duka hili litafunguliwa kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni, na Jumamosi saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana. Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma.

Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh, amesema anatarajia kuwa duka hilo jipya litakidhi mahitaji ya ongezeko kubwa la wateja wa Vodacom hasa katika jiji la Dar es Salaam.

"Tunajivunia kufungua duka hili, kwani tumetengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya. Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 30,000 wenye ajira zisizo za moja kwa moja," anasema Saleh.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. kaka michuzi waeleweshe wadau kuwa duka lililokuwa ohio street limefungwa na ndio limehamishiwa samora avenue kwenye jengo jipya la NHC Maarufu kama NHC HOUSE opposite na TWIGA BANCORP

    ReplyDelete
  2. mkitoka kazini mpite na gym japo lisaa limoja.

    ReplyDelete
  3. kwa mhahara wa laki mbili atajiajili gym gani na atamudu vipi gharama za mjini hapa??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...