Waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wamevutiwa na mafanikio yaliyopatikana kutokana na huduma ya M-Pesa nchini na kushangazwa na namna huduma hiyo ilivyofanikiwa kubadili maisha ya Watanzania. 

Timu hiyo ya wanahabari ambao wapo nchini kwa ziara ya kujifunza namna huduma ya M-pesa inavyofanya kazi wamesema huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko makubwa kwa nchi za Afrika ukilinganisha na hali halisi ya uduni wa miundombinu barani humo. 

Waandishi hao wako katika ziara ya siku nne nchini wameyasema hayo wakati wa ziara yao walioifanya katika makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania, na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kupokea maelezo ya namna huduma ya M-Pesa inavyofanya kazi. 

Kampuni ya Vodacom DRC imeanza kutoa huduma ya M pesa hivi karibuni ikiwa na mwezi mmoja mpaka sasa.
Mhariri Mkuu wa The Guardian on Sunday, Richard Mgamba(kushoto)akiongea na waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),wakati walipotembelea ofisi za The Guardian Limited,kwa kujifunza kwa ajili ya kujifunza namna ya kuelimisha jamii kuhusu huduma ya M-pesa inavyofanya kazi hapa nchini kupitia vyombo vya habari,wapili kushoto ni Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambae alikuwa mwenyeji wa wageni hao.
Meneja wa vipindi wa Clouds TV Wasiwasi Mwabulambo(kushoto)akiwaonesha namna wanavyoandaa vipindi baadhi ya waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),wakati walipotembelea ofisi za Clouds Media Group,mahususi kwa ajili ya kujifunza namna ya kuelimisha jamii kuhusu huduma ya M-pesa inavyofanya kazi hapa nchini kupitia vyombo vya habari.
Mhariri Mkuu wa Clouds Joyce Shebbe, akiongea na waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),kuhusu namna wanavyofaidika na huduma ya M pesa wakati walipotembelea Ofisi za Clouds Media Group kwa ajili ya kujifunza namna ya kuweza kuelimisha jamii jinsi ya kutumia huduma ya M pesa kupitia vyombo vya habari.
Meneja wa vipindi wa Clouds Radio Sebastian Maganga,akiwafafanulia jambo waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),kuhusu namna wanavyofaidika na huduma ya M pesa wakati walipotembelea Ofisi za Clouds Media Group kwa ajili ya kujifunza namna ya kuweza kuelimisha jamii jinsi ya kutumia huduma ya M pesa kupitia vyombo vya habari.
Meneja Mahusiano wa Vodacom DRC Fanny Kazadi,akifanyiwa mahojiano.
Mwandishi Mwandamizi wa kituo cha Televisheni cha Channel ten,Bw.Dachi Mbwana akiongea na waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),wakati walipotembelea ofisi za Africa Media Group,kwa ajili ya kujifunza namna ya kuelimisha jamii kuhusu huduma ya M-pesa inavyofanya kazi hapa nchini kupitia vyombo vya habari,wapili kushoto ni Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambae alikuwa mwenyeji wa wageni hao.
Waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao wakati walipotembelea kituo cha Televisheni cha Channel ten na Magic FM, kwa ajili ya kujifunza namna ya kuelimisha jamii kuhusu huduma ya M-pesa inavyofanya kazi hapa nchini kupitia vyombo vya habari.
Mmoja wa watangazaji wa Clouds TV Ben Kinyaiya akipozi katika picha na Mwandishi wa gazeti la Antenne A la DRC Mamy Tambu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyo fanny akija UK itabidi abadilishe jina.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...