Home
Unlabelled
zawadi ya mwaka mpya toka tanesco
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
ishu hapa siyo gharama za kunganisha tu jamani ila na uharaka wa kupata huo umeme ni muhimu. Ila pongezi kwa kupunguza gharama za vijijini.
ReplyDeletepongezi ila tuangalie pia muda wa upatikanaji wa umeme wenyewe
ReplyDeleteOk, nguzo ikihitajika bei ndio inakuwaje? au yale yale kuwa wote wajenge nyumba zako zisizi kipenyo cha umbali wa mita 30? hiyo hapo ya karibu na mita 30 nani analipia na lini? naomba nielimishwe hapa , nyumba ya kijiji ambayo ipo umbali usio zidi mida 30 toka kwenye nguzo ya umeme ipo wapi?
ReplyDeleteHatua nzuri waheshimiwa, lakini hiyo sio zawadi, hivyo ndivyo Tanesco inatakiwa kufanya kazi. Pia uhakika wa huduma hiyo ya umeme uwepo.
ReplyDeleteUshauri wa bure wa kibiashara kwa Tanesco(ushauri huu haulipiwi hata senti tano!):Lengo la Tanesco la muda mrefu na wa kati liwe,kupata wateja wengi zaidi katika kila kona ya nchi hii ili hatimaye umeme wa Tanesco uwafikie angalau asilimia 60% ya watanzania wote ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo,kutoka ailimia 12% hadi 18% ya sasa!.Kwa mantiki hiyo,hata hilo punguzo la kuunganishiwa umeme bado ni kubwa sana,lipunguzwe hadi kati ya shs.50,000/= hadi shs.100,000/=!Ningekuwa mimi ndiyo Tanesco,kitu cha kwanza ningehakikisha "nawanasa wateja wengi iwezekanavyo katika gridi yangu ya umeme",na kwa kufanya hivyo,nitajihakikishia idadi kubwa na ya uhakika ya watumiaji wa umeme wangu!nikisha kuwa na uhakika wa watumiaji,najua nitauza umeme kila siku mwaka mzima.Mapato yataongezeka zaidi,na gharama za uendeshaji kwa uniti moja ya uzalishaji na usamabazaji itapungua sana.Mtu akisha jiunga na Tanesco,sio rahisi tena kujitoa,kwasababu huduma ya umeme ni muhimu na ya lazima kwa kila mtu kwa maisha ya kisasa!Punguzeni gharama za kuunganisha wateja,ili mpate wateja wengi zaidi na zaidi,ili Mapato yenu yaongezeke mara mia zaidi,ili gharama za uendeshaji zipungue zaidi,ILI SALIO LA FAIDA KWA TANESCO liwe kubwa zaidi,na Uwekezaji mpya pamoja na Upanuzi wa huduma zenu uongezeke zaidi! that is the "economics of energy/power"!Bado shs 321,000/= ni kubwa mno kwa wakazi wa mijini kwa viwango vya sasa vya mapato ya watanzania(average monthly household disposable income),na shs 177,000/= kwa watu wa vijijini nazo bado ni kubwa sana(umaskini wa kipato vijijini unatisha,wakulima wanavuna mazao mara moja tu kwa mwaka,ambayo hayatoshelezi hata mahitaji ya kaya,below subsistence level)!Lazima tuambiane ukweli.Hivi sasa(check out on that)katika wilaya ya Sengerema,Mwanza,kuna mradi maalum wa kusambaza umeme vijijini."Nimeambiwa" kwamba,ili kuhamasisha wakazi wa wilaya hiyo wajiunge zaidi na huduma za umeme ambao nguzo zake zimeshasimikwa na zinazubiri "wateja ambao hawajitokezi kwa sababu ya kipato duni",hata punguzo la unganisho la shs.70,000/=(or less)bado limewashinda wengi!hebu nielezeni Tanesco,hivi kweli huwa mnafanya Research kabla ya kupitisha maamuzi yenu? au tunaendesha mambo yetu kwa hisia tu? kwamba Kanda ya Ziwa,wenyeji ni matajiri sana? be carefull in your analysis....
ReplyDeleteNdugu zangu TANESCO,
ReplyDeleteMAKAMPUNI YOTE DUNIANI WANATAFUTA WATEJA WAJIUNGE ILI WAUZE BIDHAA/HUDUMA ZAO, HII NDIO KAZI KUBWA YA MARKETING. WANAFANYA KILA WAWEZALO KUHAKIKISHA WATEJA WANAEDELEA KUWEPO(CUSTOMER RETENTION).
SASA NYIE MBONA MPAKA MLIPWE NDIO MUUZE BIDHAA YENU? HEBU FIKIRINI KIDOGO HII NI KARNE YA 21!
Mbona barua nzuri namna hii ila haijitoshelezi?Vipi kuhusu bei ya kuunganishiwa umeme kama unahitaji kuweka nguzo?
ReplyDeleteNa je itakuwa na urasimu kama tunavyowajua hawa jamaa au kama una vigezo vyote unawekewa? Au ni ile ya nguzo zimeisha?