April 2012
 Mzee mzima Alex Ferguson anataka kurusha ngumi mambo yanapoenda kombo, Kocha wa Man City Roberto Mancini anamwambia acha kilomolomo babu....kama si kuamuliwa wangezipiga kavu kavu laivu.....Hahahaaa aibu!
 Company wa Manchester City anafurahia baada ya kuipiga Manchester United 1-0 uwanja wa Mataa usiku huu
Kilio kwa Man U. Poleni hahahaaaaaa....
  Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabak akimkabidhi  Meneja wa masuala ya utafiti na Mazingira wa Kampuni ya Layne  tuzo ya kuwa kampuni bora kwenye masuala ya afya na usalama kazini katika sekta ya madini kwa mwaka 2011/2012. Chini ni picha ya pamoja ya Waziri na wana Layne

Ndugu,
Ujumbe huu unakujia kwa sababu naamini wewe ni blogger.Sisi kama bloggers,tunawajibika kuwa na maadili au misingi yetu.Kinyume cha hapo kazi zetu,msukumo wetu unaonekana kuwa wa kiholela kama sio kihuni.Isitoshe,ni uonevu kwa wengine.Hapa nazungumzia maadili ya bloggers.Upo mchakato unaoandaliwa ili kuwa na maadili ya pamoja zaidi.Tunausubiri kwa hamu.

Lakini wakati tukiusubiri mchakato huo utimie,nimeona nigawane nawe maarifa haya(kizuri kula na nduguyo). Ni maadili ya bloggers.Nimeyachapa katika wavu wangu.Nakuomba ufuate kiunganishi hiki:



http://www.bongocelebrity.com/2012/04/30/zingatia-bloggers-code-of-ethics/#axzz1tR0bFGyq

Mwambie na yeyote yule ambaye unadhani anaweza kufaidika na ujumbe huu.Ukiweza uchapishe katika jukwaa lako. Pamoja tutafika.

Asante na uwe na siku njema

Jeff
 Diamond akiaga kwa saluti muda mfupi kabla ya kupasua anga kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam na kuelekea kiota cha matanuzi cha Dar Live cha Mbagala
 Sio kampeni bali ni chopa iliyombeba Diamond ikitua Mbagala
Diamond akimuaga rubani wa chopa. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongoza kikao  cha Investment Forum cha The Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT)Local Investors, Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo Aprili 30, 2012.

no image
Tunapenda kuwafahamisha watu wote kuwa mafundisho ya neno la Mungu
kutoka kwa mwalimu Christopher Mwakasege sasa yanarushwa online kila
siku saa 10 na nusu usiku na kurudiwa jioni na saa 10 na nusu (saa za
Tanzania), katika link zifuatazo:

Kwa wenye PC tumia:

Kwa wenye Mac na Linux tumia:

Kumbuka ni kila siku saa 01:30GMT na kurudiwa 13:30GMT (Saa za
Marekani ni 09:30 Eastern na kurudiwa 21:30 Eastern).

Mdau Kavishe
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe akihutubia
 Habari na Picha na  Sylvester Raphael
Chama Kikuu cha Ushirika Wilayani Karagwe Mkoani Kagera, (Karagwe Development Co operative Union Ltd, KDCU) Kimefanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa ishirini na tano leo tarehe 30/04/2012 katika makao makuu ya Wilaya kwenye mji mdogo wa Kayanga katika Halmashauri ya Wilaya Karagwe.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo mkuu wa 25 wa mwaka wa KDCU Ltd alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe. Mkutano huo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa KDCU Ltd Bwana Prosper Mulungi aliyetaja madhumuni ya mkutano kuwa ni kuupitiha makisio ya bujeti ya msimu wa mwaka 2012/2013, Kufanya uchaguzi wa viongozi wapya, pia kubaini changamoto zinazokikabili chama hicho na kuzitafutia suluhu ya kudumu.
Akihutubia mkutano huo mgeni rasmi Mhe. Massawe aliwasistiza wananchi wa Wilaya ya   Karagwe kujiunga kwa wingi zaidi kwenye vyama vya ushirika ili kujiletea maendendeleo kupia vyama hivyo vya ushirika. Pia aliwashauri chama cha KDCU Ltd kuunda SACCOS ya wakulima ili wapatapo matatizo wapate sehemu ya kukimbilia kukopa na au kuweka fedha zao ili wapate faida zaidi ili kuinua uchumi wao.
Mhe. Massawe pia alitoa msistizo mkubwa juu wakulima na wanachama pia viongozi wa KDCU Ltd na viongozi wote wa serikali kuanzia ngazi ya kitongoji mpaka wilaya kusimamia usafi wa Kahawa ikidhi viwango vya dunia na kupata bei ya kumridhisha mkulima. ”Wananchi hamjali mnachanganya kahawa yenu na mavi ya mbuzi, mawe na kutokausha vizuri kahawa yenu jambo ambalo linaishusha kahawa yetu thamani katika soko la dunia.” Alisema Mhe. Massawe.
Pia Mhe. Massawe aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kutunga na kuzisimamia sheria ndogondogo (By Lwas) juu ya watu wanaofanya biashara ya magendo ya kahawa. Wanannchi wote walisistizwa kuwa walinzi wakishirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa serikali ili kudhibiti magendo ya kahawa ili serikali iweze kupata mapato na kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Karagwe.
Chama cha KDCU Ltd msimu wa 2011/12 kilifanikiwa kununua tani 4000 badala ya tani 3000 zilizokuwa zimekisiwa, pia KDCU Ltd iliweza kupata faida ya Tshs milioni 340 kwa msimu wa mwaka 2011/12. Msimu mpya ambao unaanza tarehe 01/05/2012 KDCU Ltd inatarajia kununua na kukusanya zaidi ya tani 12000 za kahawa zenye thamani ya Tshs.  14,390,000,000.=
Mafanikio mengine ya KDCU Ltd ni pamoja na kuanzisha shule ya Sekondari Nyaishozi yenye kidato cha kwanza mpaka cha sita, Imeanzisha Hoteli ya Kisasa mjini Bukoba (Coffee Tree), Imeanzisha kiwanda cha kukoboa kahawa na kufunga mashine mbili za kuchambua kahawa katika madaraja (Grading Mashine), kuanzisha kitengo cha kutafuta masoko ya kahawa nje ya nchi ili kuboresha bei ya kahawa kwa mkulima, kupata cheti cha mradi wa kilimo hai ‘Organic’.
Changamoto kubwa zinazokikabili chama cha KDCU Ltd ni bei katika masoko kubadilika mara kwa mara, wakulima kutoa kahawa isiyokidhi viwango vya ubora wa kahawa duniani, pamoja na vyama vya msingi kutokuwa na fedha ya mtaji ya kujiendesha vyenyewe.
Mkutano Mkuu wa KDCU Ltd ulihudhuriwa na wajumbe wake zaidi ya 230 kutoka katika vyama vya msingi 76 vinavyounda chama kikuu cha KDCU Ltd. Pia mkutano huo ulihudhuliwa na wageni mbalimbali kutoka wilayani na nje ya wilaya katika Vyama vingine vya ushirika mkoani Kagera. 

 Washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Ustawi wa Jamii 2012 wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu wao,Mary Boniface (katikati) wakati wa mazoezi ya kujiandaa na shindano lao linalotaraji kufanyika siku ya ijumaa (Mei,4 2012),ukumbi wa Maisha Klab jijini Dar es salaam.
 Warembo wa Redd's Miss Ustawi wa Jamii 2012 wakiwa kwenye pozi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA) Bw. Nicholaus Mgaya leo baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi zinazofanyika kitaifa mkoani humo.
Na Pardon Mbwate na Felister Chubwa wa Jeshi la Polisi Kigoma

 Askari Polisi mmoja wa Kikosi cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Kostebo Shaban Hamisi Gobeka(37), amefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokua akiendesha kuacha njia na kugonga mti kushoto pembeni mwa barabara ya Lumumba mjini Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishns Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 12.15 jioni katika mtelemko mkali eneo la Lubengela wakati askari huyo akiendesha pikipiki yenye namba T.757 BYY aina ya Toyo akitokea Mwanga kuelekea Kigoma mjini.

Kamanda Kashai amesema wakati wa ajali hiyo Kostebo Gobeka mwenye namba F. 1561 alikuwa amempakia kijana mwingine aitwaye Filbert Kibuka(25) mkazi wa Mwanga mjini Kigoma ambaye yeye amejeruhuwa vibaya na amelazwa katika Hospitali ya mkoa Maweni kwa matibabu zaidi na hali yake imeelezwa kuwa ni mbaya.

Amesema ingawa Polisi bado inachunguza chanzo cha ajali hiyo, lakini imebainika kuwa imesababishwa na mwendo kasi uliotokana na kukatika kwa bleki ya pikipiki hiyo huku ikiwa kwenye mteremko mkali.

Kamanda Kashai amesema Konstebo Gobeka alikuwa ni dereva wa kutumainiwa wa pikipiki za Polisi na alipata mafunzo ya uendeshaji wa pikipiki ambapo kabla ya kuhamishiwa kikosi cha mawasiliano ya Polisi mkoani hapo, marehemu alikuwa ni miongoni mwa askari waliokuwa wakiendesha pikipiki za doria mkoani Kigoma na hakuwa na kumbukumbu zozote za ajali.

Hata hivyo Kamanda Kashai amesema Jeshi la Polisi limempoteza Askari shupavu na mchapakazi lakini pia amesema pikipiki aliyopatanayo ajali Askari huyo haikuwa mali ya Jeshi la Polisi.

Taarifa hii imehaririwa na kusambazwa kwenu na Insp. Mohammed Mhina, Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar.
Makamu wa Rais, Dr. Mohamed Gharib Billal (kulia) na Balozi wa Korea,Mh. Young Kim wakikata utepe kuzindua Chuo cha Ufundi Veta,Mkoani Manyara kikiwa ni Chuo pekee kilichopo mkoani Manyara. Mkoa huo ni moja ya mikoa mipya ambao hauna chuo kingine chochote cha elimu yoyote zaidi ya hiki chuo cha Veta kilichozinduliwa leo.Uzinduzi huo, uliofanyikia katika mji wa Babati, umefanywa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Mohamed Gharib Bilal aliyeandamana na Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Philip Mulugo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Eng. Zebadiah Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi akimuonyesha Makamu Rais, baadhi ya zana za kilimo zitakazotumiwa na Chuo kipya cha Veta Mkoani Manyara.
ELIGRETA RAYMOND (Mama Niwajwa).
1936 – 2011

Mama Mpendwa,Zimepita Siku, Miezi na leo hii 30.4.2012 imetimia mwaka mmoja toka tulipokupumzisha katika nyumba yako ya milele. 

Ingawaje umetutoka kimwili, Kiroho bado tuko pamoja. Tunasikia sauti yako ya upole ikiita na kutufariji kama vile kuku akumbatiavyo viranga vyake. Hakika pengo ulilolicha halitazibika.

Unakumbukwa sana na watoto wako,kaka zako, wakwe zako, wajukuu wako ndugu jamaa na marafiki.

“Bwana alitoa na Bwana ametwaa"

The Raymond’s Mchani Family (Kisangara Mwanga Kilimanjaro)
Mkurugenzi mpya wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA) Tumaini Mwailege akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa kupigania mazingira mazuri ya kazi na maslahi bora kazini. Mwailege ameanza kufanya kazi rasmi leo (1/5/2012) amechukua nafasi ya Rose Haji aliyemaliza muda wa utumishi wake katika taasisi hiyo mwaka jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mohamed Tibanyendera akifuatiwa na Mjumbe wa bodi Elias Mhegera.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA) Mohamed Tibanyendera akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi mbalimbali za kuhakikisha kuwa taaluma ya habari inaimarika hapa nchini huku Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Tumaini Mwailege akimsikiliza.



Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka (kushoto), akimkabidhi tuzo Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda, baada ya kampuni hiyo kushinda masuala ya usalama mahali pa kazi, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama kazini duniani, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Makongoro Mahanga.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) akimpongeza , Renatus Nyanda kwa niaba ya TBL.
Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Kabaka pamoja na baadhi ya washindi wa tuzo hizo.
The the Africa Leadership Initiative East Africa (ALI-EA), held its graduation ceremony today for its 2010 Fellows, with calls for the graduates to play their role in transforming the African continent by putting into practice the leadership lessons they have learned during their two-year journey together in pursuit of leadership excellence.

Ali Mufuruki, Chairman and Founder of ALI EA reminded the fellows of their responsibility to society, saying that the future of East Africa and indeed of the African continent depends on the quality of its leaders and the choices they will make on behalf of their people.

"We selected you to join this program because we believed that each and every one of you has within them the qualities of a great leader. Our purpose was and remains that of helping you to recognize and come to terms with that reality and the implied responsibility. " Mr. Mufuruki said in his welcome address.

"This programme was designed to equip you with the tools you will need to face up to the responsibility of leading and by that I mean leading well. We have brought you together in this group so that you know you are not alone and have unlimited access to a vast network of resources you can rely on for useful feedback and wise counsel, a network of leaders whose values you share. So let's go and do the work that awaits us with the confidence that derives from knowledge and the urgency the work demands" Mr. Mufuruki added.

Speaking during the graduation ceremony at the Mt Kenya Safari Club in Nanyuki, Kenya, the African Development Bank President, Dr. Donald Kaberuka urged the fellows to take on the challenge of transforming the immense opportunities that Africa has into real possibilities so that future generations of Africans can live dignified lives and claim their rightful place in the in the global community of nations.

"The majority of African countries attained independence from their colonial rulers long before most of you were born. Half a century later, there is broad agreement Africa is turning the corner, building a new momentum. My view is that the challenge of the leadership now is how to sustain the momentum. It is for this reason that I am very pleased to be here to bear witness to a process of leadership development that gives me hope of a better future for our continent." said Dr. Kaberuka.

"I want you to know that in me and the institution I lead, ADB; you have a partner you can call upon whenever in need and please do so without hesitation. Our support for and partnership with the Africa Leadership Initiative (ALI) East Africa emanates from our firm belief in that tackling the leadership problem in Africa is key to the successful turnaround of our continent's fortunes. I wish you all the best and look forward to engaging with you individually and collectively in the days and months ahead." he added.

The fellowship comprises four seminar spread over a two-year period. During the seminars, fellows engage in Socratic conversations on various issues reading from classical and contemporary texts under the careful watch of expert moderators. 

The themes of the seminars include a study of leadership styles and a search for the fellow’s own moral compass and appreciation of how it affects their exercise of authority; a search of the Good Society (going back in history to understand the evolution of human societies, the political, cultural and spiritual structures that underpin them, sources of strength and instability, etc.); a look at the challenges of leading in an era of Globalisation, understanding the challenges leaders are facing in today’s fast changing, connected and increasingly interdependent world defined by rapid technological, economic and societal changes and finally a study of the balance between self and society, encouraging fellows to think about their own legacies.

The Fellows also commit to carrying out a high-impact Leadership Project of their own choosing and design vetted and approved by their peers.

The 2010 Fellows whose class is aptly named "UWEPO" meaning "presence" in Kiswahili, are:

Stella Kilonzo, Chief Executive of Capital Markets Authority of Kenya, Magnus Mchunguzi, Vice President Commercial & MD of Ericsson South Africa; Awel Uwihanganye, Managing Partner of Tetea Uganda; David Mpanga, Partner, Kampala Associated Advocates; Dr Laila Macharia, Principal of Scion Real, Kenya, Richard Mugisha, Managing Partner, Trust Law Chambers of Rwanda; Leslie Rance, Head of corporate and regulatory affairs at British American Tobacco, Southern Africa Region; Andrew Rugege of Rwanda is Africa Regional Director of ITU and ITU Rep to the UN ECA in Addis Ababa, Ethiopia; Winnie Ouko, Managing Director, Lattice Consulting Limited of Kenya; Mugo Kibati, Director General, Kenya Vision 2030 Delivery Secretariat; Pauline Mbayah, Director, ATMS Foundation, Johannesburg, South Africa; Jeremy Awori, MD and CEO, Standard Chartered Bank Tanzania Ltd; Rosette Chantal Rugamba, Founder, Songa Africa of Rwanda; Davith Kahwa, Founder, President & CEO, Equip Advisory Group (Pty) Limited of Tanzania; Frederick Kitaka-Mutebi, Co-Founder & Director of Finance, Quality Chemicals Ltd of Uganda and
Rehmah Kasule, Founder and CEO of Century Marketing Uganda.

One fellow Dr. Alwyn Mziray of Tanzania passed away suddenly in early 2011. May the Almighty rest his soul in eternal peace.
no image
Amazing ............................

1. Both Dr. Kenneth Kaunda and Dr. Kamuzu Banda were longest serving
President's of both countries and their roots are somehow not traced
from Zambia and Malawi, respectively. Both Kaunda and Kamuzu, having a
common slogan of "Wamuyaya" (Forever), had something to carry in their
hands as a symbol of Authority.

2. FTJ Chiluba, born in 1943, took over from Kenneth Kaunda and Bakili
Muluzi,born in 1943, took over from Kamuzu Banda. Both Chiluba and
Muluzi went on to seek a 3rd term of office but failed after extreme
opposition to both bids.

3. FTJ Chiluba  brought in Levy Mwanawasa and campaigned for him single handedly; Bakili Muluzi brought in Bingu wa Mutharika and campaigned for him single handedly


4. Both Mwanawasa and Mutharika won those elections.

5. Shortly after being elected as President, Mwanawasa fell out favour
with Chiluba and dragged him to court over corruption; Shortly after
being elected as President, Mutharika fell out favour with Muluzi. The
new Malawian President took his predecessor to court over corruption.


Now it gets interesting - Chiluba was prosecuted by the Mwanawasa
administration and Muluzi was prosecuted by the Mutharika
Administration. Mwanawasa won a 2nd Term of office, Mutharikha won a
2nd Term of office. Mwanawasa chose Rupiah Banda as Vice President,
Mutharika chose Joyce Banda as Vice President. Mwanawasa
 died in his 2nd term of Office due to Cardiac Arrest, Mutharika died
in his 2nd term of Office due to Cardiac Arrest (both deaths were
predicted by TB Joshua).

6. Rupiah Banda took over from Levy Mwanawasa due to death of
incumbent; Joyce Banda has taken over from Bingu wa Mutharika due to
death of incumbent.The people who took over from the dead Presidents
in both countries are named "Banda"!

7. Aftr 3yrs, President Banda in Zambia lost to veteran opposition
leader Michael Sata. Joyce Banda who has taken over the Presidency
will face election in 2014 which will make her serve 3 yrs, will she
lose to veteran John Tembo??
Serengeti Breweries Limited (SBL) is pleased to announce the appointment of Mr. Steve Gannon as Managing Director, effective 1 July 2012. Mr. Steve Gannon joins SBL from Diageo Cameroon Hub where he has been Managing Director since 2009. In this role at the helm of SBL, Mr. Gannon will be a member of the East African Breweries Ltd Executive committee.

Under Mr. Gannon’s leadership for three years, the Diageo Cameroun Hub business has delivered significant share growth in beer and established new businesses in premium spirits. During Mr. Steve Gannon’s tenure leading the Diageo Cameroun Hub business he has led significant investment behind building capacity and expanding the businesses routes to market. 

In addition, Mr. Gannon has been central in leading the development of the Business Coalition Against Corruption in Cameroon – an unprecedented initiative in partnership with the Cameroon government to create a private sector movement united against corruption. 

Prior to his role within Diageo Cameroun Hub, Mr. Steve Gannon has had 30 years commercial experience in Diageo, including leading the Diageo Venture Africa Business, launching the Guinness brand in a number of African markets as well as doubling the Diageo Africa spirits business in the Diageo Venture Africa markets. 

Issue by :
Teddy Mapunda
Corporate Relations Director.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wajiandaa na uzinduzi wa klabu ya michezo kwa watumishi wake ili kuwapa fursa ya kulinda afya zao na magonjwa mabalimbali yanayotokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya kila siku kama vile kisukari, shinikizo la damu na mengineyo mengi ambayo kwa kwa sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya binadamu wa leo.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Oyesterbay Meneja wa timu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu na utawala bi Jane nchimbi alisema 'Tumekuwa na utaratibu huu tangu mwanzoni mwa mwaka jana lakini kidogo tulikuwa tumebanwa na majukumu ,lakini kwa sasa tumeamua kwa pamoja kuufanya utaratibu huu kuwa endelevu kwani utasaidia kujenga afya hasa ikizingatiwa kuwa watumishi wengi wa umma tunatumia muda mwingi kwenye ofisini tukihudumia wateja hivyo kuwa na nafasi finyu kushiriki mazoezi kama ambavyo NHIF tumethubutu...

Mpango huu unawajumuhisha pia wale watumishi wa Mfuko kwenye ofisi za Mkoani, mpango wa baadaye ni kuwa na eneo maalum la kufanyia mazoezi (gym) ili huduma zote za msingi ziweze kupatikana.alisema Bi Jane kijazi

Naye nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NHIF bi Sabina Komba ……aliwataka wafanyakazi wanaoshiriki mazoezi kwenye klabu hiyo kutambua kuwa wao ni mabalozi katika kuhamasisha wananchi na wananchama wa mfuko huo kupenda na kuthamini michezo kwani mfumo wa maisha ya kisasa umegubikwa na maradhi mengi na makubwa ambayo yanaathiri afya zetu na walio wengi
no image
Na Mary Ayo,Arusha


VYUO Vikuu Afrika Mashariki vimetakiwa kuwafunduisha wanafunzi wao mafunzo ya ujasiliamali na masomo yanaoendana na mahitaji ya soko la ajira la Afrika Mashariki.


Wito huo ulitolewa na mwenyekiti wa Umoja wa Waajiri Afrika Mashariki, Jackline Mugo kwenye uzinduzi rasmi wa umoja huo uliofanyika jijini hapa mwishoni mwa wiki.


Alisema waajiri wengi katika ukanda wa Afrika mashariki wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo kutopata wafanyakazi walioiva kwenye maeneo yao ya kazi.


“Hii ni moja tu ya changamoto nyingi tunazokumbana nazo katika utendaji wetu wa kila siku kama waajiri na hivyo tunaamini kupitia mwamvuli huu tutaweza kukaa pamoja kama waajiri na wadau wengine kupata suluhisho la matatizo yetu.” Alisema Mugo.




“Wanafunzo wanaomaliza vyuo wanatakiwa kuivishwa vya kutosha kabla ya kuingia kwenye soko la ajira,” alisema na kuongeza: “Waajiri wanamchango mkubwa kwenye kuimarisha mtangamano wa Afrika Mashariki kutokana na mchango wao katika nchi wananchama.”


“Kupitia mwamvuli huu, tunaweza kuishauri serikali juu ya namna ya kuboresha mambo mbalimbali ili kukuza na kudumisha mtangamano wetu.”


Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Afrika Mashariki, Musa Sirma alilipongeza jukwaa la waajiri kwa kuja na mkakati wao wa namna ya kudumisha mtangamano wa Afrika Mashariki.


Sirma ambaye ni Waziri wa masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Kenya alisema jukwaa hilo limekuja katika wakati muafaka ambapo jumuiya inatekeleza itifaki ya soko la pamoja.


Alisema jumuiya itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa waajiri wanafanya kazi yao katika mazingira bora na hatmaye kudumisha mtangamano.


Alisema waajiri ni sekta muhimu katika jumuiya kwa kuwa wao ni waajiri wakubwa wa watu wa Afrika mashariki na kulipa kodi mbalimbali zinazozifanya nchi zetu kujiendesha.


Umoja huo wa waajiri ulianzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kukuza uzalishaji na kuongeza ushindani wa kibishara Afrika Mashariki.
Wanachama wa UWF wakiwa na baadhi ya washindi wa waliong'ara vizuri kwenye shindano la kumsaka Mwanamke Mjasiliamali,kupitia tuzo ya Mwanamakuka (lililofanyika March 8),na hatimaye kuwapata washindi watano wa tuzo hiyo.(KUONA TUKIO ZIMA LILIVYOFANYIKA BOFYA HAPA).
Meneja Miradi wa UWF,Bi.Mariam Shamo akimkabidhi Bi Nassra Mussa  hundi ya shilingi laki tano kwa kuibuka mshindi wa tano wa shindano la Mwanamke Mjasiliamali (tuzo ya Mwanamakuka).Pichani kulia ni  Mwenyekiti wa UWF,Bi Mwate Madinda.Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za UWF zilizopo Mikocheni, jijini Dar
Muwakilishi wa Clouds FM,Abdull Mohamed akimkabidhi Bi.Joyce Mabula hundi ya shilindi laki saba unusu kwa kuibuka mshindi wa nne wa tuzo ya Mwanamke Mjasiliamali (tuzo ya Mwanamakuka). 
Baadhi ya Washindi wa shindano la Mwanamke Mjasiliamali kupitia tuzo ya Mwanamakuka wakifuatilia jambo
Meneja Miradi wa UWF,Bi.Mariam Shamo akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za UWF zilizopo Mikocheni, jijini Dar.
Mwenyekiti wa UWF,Bi Mwate Madinda akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo sambamba na wanachama wenyewe wa UWF.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa mabati 264 kwa sheha wa Stahabu-pemba bw haji Faki Komb ikiwa ni msaada wa Airtel kushiriki kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali za maeneo ya STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI. Katika hafla hiyo Airtel ilijitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao vyote vyenye thamani ya 10/-tsh ili kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha Michenzani pemba mwishoni mwa wiki. Kati mwenye shati la drafti akishudia ni Afisa Mipango wa Wilaya Mkoani Bw Omar Shehe Omari na anaefuata ni Sheha wa Michenzani Bw Abdalah Omari.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa Nondao 62 kwa Sheha wa Michenzani Mzee Abdalah Omari huko Pemba visiwani ikiwa ni msaada wa Airtel kushirikiana na wananchi wa Tanzania visiawani kwaajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali za maeneo ya STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI. Katika hafla hiyo Airtel ilijitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika vyote vyenye thamani ya 10/-tsh ili kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha Michenzani pemba mwishoni mwa wiki. Naeshudia kati mwenye shati la drafti ni Afisa Mipango wa Wilaya Mkoani Bw Omar Shehe Omari.

Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiana na jamii sehemu mbali mbali kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kisiwani pemba maeneo ya michenzani kitakachosaidia kutoa huduma maeneo ya STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI.

Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa Airtel Zanzibar Bw Hagai Samson alisema “msaada huu wa Airtel kwa wakazi wa huku pemba hautaishia hapa , leo tumejitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika kumalizia ujenzi wa kituo hiki cha afya tukiwa na imani vikitumika kwa usahihi vitasaidia kuboresha huduma za afya katika maene ya Michenzani, Chokocho, Kizumgu,Kandandarani na Shidi.

Airtel Tanzania tunawashukuru sana wateja wetu mliopo pemba kwa kuwa ndio hasa wanaotuunganisha na jamii hii siku ya leo. Tunachojitolea hapa ni sehemu ya faida tunayoipata kila mnapozitumia huduma zetu zikiwepo kupiga na kupokea simu, Airtel money pamoja na huduma yetu ya Internet ya 3.75G.

Kwa upande wake Sheha wa Michenzani akipokea msaada huo wa vifaa vya ujenzi wa kituo hicho cha Afya aliishukuru Airtel na kuwaomba wadau wengine wanaofanya biashara kisiwani huko kuiga mfano huo wa Airtel.

“ naishukuru sana Airtel kwa msaada wao huu, utatusaidia sana kukamilisha ujenzi wa kituo hiki cha Afya hapa michenzani, tunaamini hii ni jitihada za kumuunga mkono Mheshimiwa raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh, Ally M. Shein ambae wiki moja iliopita aliweka jiwe la msingi katika kituo hichi na kuhimiza ujenzi wa kituo hiki uende kwa kasi ili kusaidia kupunguza adha ya mrundikano wa wagonywa katika kituo kimoja kile cha Bogoa.

Nae Afisa Mipango wa Wilaya ya Mkoani Omari Shehe Omari akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ujenzi wa kituo hicho cha Afya una lengo la kupunguza matatizo ya afya yanayoikabili jamii inayoishi maeneo hayo hasa kwa kuzingatia wakina mama na watoto.

“Ninaipongeza Airtel sana kwa kujitolea na kutusaidia kufikia malengo yetu ya Milenia, sisi tuna dhamira ya kuboresha Afya na elimu kwa pamoja, kila Skuli iwe na kituo cha Afya au kila Shehia (Serikali ya Mtaa) iwe na kituo chake cha Afya.

Hivyo kwa msaaada huu utasaidia sana serikali yetu kutifika malengo yake kwamba pia michenzani watapata kituo chao hapa karibu.”

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ina mkakati wa kutoa misaada ya kijamii kwa kugusa sekta za mazingira, Elimu na Afya kwa lengo la kuisaidia serikali na jamii kwa ujumla kupambana na changamoto mbalimbali .

Mwaka huu wa 2012 pia Airtel imejipanga kuhakikisha jamii iliyopo pembezoni mwa nchi mbali na kupata huduma bora ya mawasiliano ikiwemo ile ya Airtel money pia itashiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ili kujenga vyema ushirikiano na jamii kama ilivyoshiriki kuboresha miundombinu ya Afya Visiwani Zanzibar.
no image
Wiki iliyopita nilikuwa kwenye ofisi ya Jumuiya yetu nikiongea na baadhi ya vijana waliowasili hivi karibuni kutokea “UBATANI”(Hili ndilo jina tulitumialo badala ya “UTURUKI”kama vile litumikavyo jina “UMANGANI” badala ya “UGIRIKI” )

Ilijionesha wazi katika mazungumzo yetu kuwa picha waliyokuwa wakiidhania ilikuwa ni tofauti mno na hali halisi waliyokumbana nayo.Baadhi yao wamekuja na seaman book wakitegemea wangepata kazi ya melini mara tu watapofika!!!

“Niliambiwa nikifika Umangani kuna meli kibao zinatafuta mabaharia na mshahara ni buku!!!Lakini tangu nimefika hapa nimegundua kuwa zilikuwa ni kamba tu za washkaji maana hata huko bandarini si rahisi kukaribia”Alisema mmoja wa vijana hao kwa unyonge na uchungu.

Mwingine aliongezea akikuna kichwa “Nimelazimika kuomba msaada kwa washkaji zangu waliopo UK ili nitafute mchongo wa kuchomoka maana hali nilivyoiona sivyo nilivyoambiwa na hadi sasa washkaji wenyewe wananipa story tu”

“Mimi rumba nililishtukia tangu pale tulipokuwa tunabinjuka toka ubatani baadae tukakamatwa na kuwekwa kambini,Walipotuachia tuje Athens nikampigia simu mama anitafutie tiketi ya kurudi!!!!Alisema kijana aliyekiri kuwa hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kusafiri nje ya nchi.

Nimelazimika kuielezea mifano hai hiyo nikiwa sina lengo la kufichua siri za jandoni,bali niweze kupata nafasi ya kutoa picha kwa wale wanaopanga kufuata njia hizo hizo bila ya kuwa na picha kamili ya hali halisi itayowakabili ambao wengi wao hawana ule ubavu wa kukabili mazingira kama walivyoyakabili wasafiri wa zamani ambao walivumilia mengi magumu zaidi ya haya.

Namalizia kwa taarifa ifuatayo:

Serikali ya hapa imepitisha bungeni hivi karibuni sheria ya kuanzisha kambi za kuwahifadhi wageni wanaoingia nchini kinyume cha sheria. Kuanzia sasa wageni wakibinjuka hawatakuwa wanaachiwa waende Athens, badala yake watahifadhiwa (WATAFUNGWA) katika kambi hizo hadi pale utapopatikana uwezekano wa kuwarudisha makwao.

Tunawaomba vijana wote wataofikiria kupitia njia hizi walijue hili, ili wasije wakawatia presha wazazi wao pindi watapokuwa wamefungwa na hatimae kurudishwa.

Niliyoyasema si vitisho bali ni wajibu wetu kuwajuza ndugu zetu wa nyumbani wasioijua hali halisi ya huku na baada ya hapa wao wana haki ya kuamua kuja au kutokuja. .

Kwa kuhakiki maelezo niliyoyatoa kuhusu kambi za kuwafungia wageni wanaweza kuingia google kabla hawajaamua kuja.TAARIFA YA MWISHO NI KUWA WAMEPELEKWA WAGENI 56 KATIKA KAMBI MPYA ILIYOPO KIJIJI CHA AMYGDALEAS.ITAYOKUSANYA WAGENI 1,200.

Ahsanteni

KAYU LIGOPORA

KATIBU MKUU JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI