Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii na kuthibitishwa kutoka katika vyanzo vyetu vya habari, inaeleza kuwa Msanii aliyekuwa akisumbuliwa kiafya kwa muda mrefu,afahamikae kwa jina la Sadick Juma Kilowoko Maarufu kwa Jina la Kisanii SAJUKI Amefariki Dunia mapema leo asubuhi.
Marehemu Sajuki, ambaye hivi karibuni Serikali ilijitolea kubeba jukumu la kugharamia matibabu yake na hatimaye hivi karibuni kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili,amefariki Dunia mapema leo majira ya saa moja.
Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi-Ameni.
Wadau tutazidi kutaarifiana kwa habari nyingine kuhusiana na msiba huu kwa kadiri zitakavyokuwa zikipatikana.
Rest in peace Sajuki. innallah wa inailaah raajun.
ReplyDeleteR.I.P sajuki,roho inaniumaje
ReplyDeletePoleni sana wafiwa mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi Amen
ReplyDelete
ReplyDeleteRIP BROTHER. NA MUNGI AMPE MKEO NGUVU YA KUSIMAMA IMARA KIROHO NA KIMWILI KTK HIKI KIPINDI KIGUMU.
Bwana ailaze roho ya marehem pahala pema peponi, amen
ReplyDeleteR.i.p. kaka
ReplyDelete