Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi
wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja
jana,ujenzi huo umejenga na Kampuni ya Mecco kwa umefadhiliwa na Benki
ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi,ikiwa ni shamra shamra ya
kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akizungumza na Wananchi na
wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,sherehe za
ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini
Unguja,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya
Kandiero,wakikata utepe kufungua Barabara ya
Mfenesini-Bumbwini,iliyojengwa na Kampuni ya Mecco kwa ufadhili wa
Benki ya Dunia kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ikiwa
shamra shamra za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) Mwakilishi wa ADB Tanzania
Toniya Kandiero,(wa pili kulia) Naibu Waziri wa Mindombinu,Mawasiliano
Issa Haji Gavu,(wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Miundombinu
,Mawasiliano,Dk.Juma Malik Akili,(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa
Kasakazini Unguja Pembe Juma,(kushoto) wakitembea katika Barabara ya
Mfenesini-Bumbwini baada ya kufunguliwa Rasmi jana,ikiwa ni shamra
shamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa
akizungumza nao katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya
Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja,katika kuadhimisha miaka
49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Swali la kizushi tu:katika hali ya kawaida,zaidi ya asilimia 60% ya Mapato yote ya Zanzibar,yalipaswa yatokane na Ushuru wa Forodha kwa bidhaa zote ziingiazo Bandari ya Zanzibar kutoka nchi za Nje,na kodi zingine za bidhaa kwa bidhaa zote zitokazo Zanzibar kuja Tanzania Bara au kwingineko!Swali langu linakuja hivi,"Je,Zanzibar inayapata Mapato hayo kwa ukamili wake kama inavyostahili?".Na,je,bidhaa zilizo kwisha tozwa kodi Zanzibar,bado lazima zitozwe tena kodi ziingiapo bandari ya Dar es salaam?.Kabla sijaendelea na swali lifauatalo,naomba,mtanzania yeyote mwenye uelewa sahihi na majibu ya uhakika(sitaki uzushi)atupatie maelezo muafaka hapa ili tuelimishane!Nina makusudio yangu,mazuri tu kwa pande zote mbili,ambayo nitakuja yaeleza!tuwe na subira!
ReplyDelete