Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana,ujenzi huo umejenga na Kampuni ya Mecco kwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi,ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akizungumza na Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya Kandiero,wakikata utepe kufungua Barabara ya Mfenesini-Bumbwini,iliyojengwa na Kampuni ya Mecco kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ikiwa shamra shamra za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya Kandiero,(wa pili kulia) Naibu Waziri wa Mindombinu,Mawasiliano Issa Haji Gavu,(wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Miundombinu ,Mawasiliano,Dk.Juma Malik Akili,(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kasakazini Unguja Pembe Juma,(kushoto) wakitembea katika Barabara ya Mfenesini-Bumbwini baada ya kufunguliwa Rasmi jana,ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Swali la kizushi tu:katika hali ya kawaida,zaidi ya asilimia 60% ya Mapato yote ya Zanzibar,yalipaswa yatokane na Ushuru wa Forodha kwa bidhaa zote ziingiazo Bandari ya Zanzibar kutoka nchi za Nje,na kodi zingine za bidhaa kwa bidhaa zote zitokazo Zanzibar kuja Tanzania Bara au kwingineko!Swali langu linakuja hivi,"Je,Zanzibar inayapata Mapato hayo kwa ukamili wake kama inavyostahili?".Na,je,bidhaa zilizo kwisha tozwa kodi Zanzibar,bado lazima zitozwe tena kodi ziingiapo bandari ya Dar es salaam?.Kabla sijaendelea na swali lifauatalo,naomba,mtanzania yeyote mwenye uelewa sahihi na majibu ya uhakika(sitaki uzushi)atupatie maelezo muafaka hapa ili tuelimishane!Nina makusudio yangu,mazuri tu kwa pande zote mbili,ambayo nitakuja yaeleza!tuwe na subira!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...