Home
Unlabelled
Jengo jipya la kuhifadhia maiti katika hosptali ya Bombo mkoani Tanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hata Tanga jamani mnatumia kiswahili butu namna hii kwa nini isiwe 'Chumba cha kuhifadhi Miili' au 'Chumba cha kuhifadhi Marehemu'
ReplyDeleteMdau
Mombasa
Mbona kuna saraba kubwa?
ReplyDeleteMdau hapo juu wewe ndiyo ambaye hujuwi kiswahili..neno MAITI lipo sawa kabisa na wala si TUSI na wala halina maana mbaya.Neo MAITI ni jina analopewa mtu anapofariki na limetokana na neno la lugha ya Kiarabu MAYIT likiwa ni mnyumbuliko wa neno Mawt( yani Mauti kwa Kiswahili).Mtu akiwa anaoumwa haitwi mtu anayeumwa anaitwa MGONJWA ni jina jipya analopewa mtu aliye katika hali ya ugonjwa.
ReplyDeleteNaungana na anon wa jan31,12:40:00 am
ReplyDeleteUnapaswa kuelewa kuwa Maiti si mwili tuu Bali mwili uliokufa sasa utakaposema umehifadhi mwili hapo huoni utaleta Sintofahamu katika lugha husika. Ila marehemu laweza pia kutumika kwani ni jina la mwili au mtu aliyepoteza uhai. Upo hapo?
Mwili wa marehemu 'A' umehifadhiwa hospitali.
ReplyDeleteMaiti ya Marehemu 'A' imehifadhiwa hospitali.
Sentensi ya mwanzo inaonesha heshima kwa marehemu kwa 'A' kwa kufuata tamaduni za Afrika Mashariki.
Hivyo chumba cha kuhifadhi miili ya marehemu ni bora kuliko nyumba ya kuhifadhi maiti kuhifadhi maiti.
Mali ya marehemu ni sahihi zaidi kuliko mali ya maiti. Tukumbuke marehemu wana 'roho' na ndiyo maana tunawafanyia tambiko, sala au swala.
Marehemu ni wa jinsia gani na siyo maiti ni ya jinsia ipi.
Tuwahifadhi marehemu au miili ya marehemu kwa staha inayostahili iwe kaburini, hospitali au katika tanuru la ki-hindu n.k
Marehemu linatumika pindi unapomtaja mtu wakati mnapokumbuka mambo aliyoyafanya au mnapomzungumzia hivyo chumba cha kuhifadhi maiti ni sawa but chumba cha kuhifadhi marehemu (si sawa)
ReplyDeleteHILI NENO "MWILI" LIMEZUKA HIVI KARIBUNI WALA SIJUI CHANZO CHAKE KILITOKA WAPI.
ReplyDeleteCHUMBA CHA MAITI NI SAWA KABISA. TOKA UTOTONI MIMI NAJUA HIVYO.
MDAU WA KWANZA UNATAKA KUTUCHANGANYA, "CHUMBA CHA KUHIFADHIA MIILI"???!!! MIILI IPI? AU "CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAREHEMU" YUPI???!!!
HII INANIKUMBUSHA KISWAHILI CHA "NTAKUSUBIRI LISAA LIMOJA" !!!!! BADALA YA NTAKUSUBIRI MUDA WA SAA MOJA
Nitakusubiri kwa muda wa saa moja ni sahihi zaidi ya Ntakusubiri muda wa saa moja.
ReplyDelete