Katika pita pita za Kamera man wa Globu ya Jamii,alikatika maeneo ya Katikati ya Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam na kumnasa jamaa akijitahidi kukausha maji yaliyokuwa yametuama katika kidimbwi kilichopo katikati ya njia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa hapa jijini.Mpaka Kamera man wetu anaondoka katika eneo hilo alimuacha jamaa huyo akiendelea na kazi yake hiyo japo baada ya muda kidogo mvua ilinyesha tena,sasa sijui alichukua uamuzi gani baadae.
Home
Unlabelled
kwa usafi huu mbona Bongo Tambarareeeee.....!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Watu wana utani, ni heri kurudi kijijini. Yaani mtu mzima na akili zake anapoteza siku nzima kufanya huo upumbafu! Nauita upumbafu kutokana na hata kifaa anachotumia kukaushia hayo maji hivi ni gunia la deki au???? Mi nafikiri anaosha hayo magari. Hivi Michuzi hukumuuliza hicho anachokifanya hapo nisahihi au ndio kupoteza muda? Halafu mwisho wa siku analipwa kwa kazi hiyo au amejitolea? Watanzania hadi tuamke kazi kweli kweli......
ReplyDeletendugu anonymous hapo juu, hawa jamaa sio wanafanya usafi kivile ...! hawa jamaa ni wauza either nyanya au viatu vya mitumba. yani ni aibu kuona nguvu kazi inasugua sugua viatu na kuuza hasa pale samora avenue ktkt jengo la kitega uchumi.hivi kweli inakuingia kichwani kuwa mtanashati kama yule anakubali kukaa na uchafu wa maji na mazalio ya mbu anafanyia biashara hapo na diwani yupo???? ... inasikitisha kuona serikali inafumbia macho na kuwaita wajasiriaa mali. bado wengi wamelala! asante michuzi kututonesha
ReplyDeleteHuyo anategea na sio ari ya kazi kwa kujituma kwa ridhaa.
ReplyDeleteSi ajabu baada ya muda ataanza kuwatoza ada wanaopita na magari kwa kigezo yamkuwa anasafisha maji ili njia ipitike kwa magari!
wewe mtowa maoni wa mwanzo hivi ni nani mbumbavu hapo? jamaa kapewa kazi afanye na anafanya mwisho wa siku analipwa upumbavu kwa upande wa wake ni nini?
ReplyDeletewapumbavu ni pamoja na wewe na comments zisizoeleweka pamoja na wahusika waliomuajiri huyu jamaa na ambao wameshindwa kumpa vifaa vya maana au kutatua tatizo lililopo hapo.
kuwa mstaarabu na wacha kuita wenzako wapumbavu.